Comoro kushirikiana na Tanzania katika sekta za kimkakati asema Rais Azali Anena
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazumgumzo na Rai...
SERIKALI YAWEKA MPANGO MKAKATI MAALUM WA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA MALARIA NCHINI
Written By CCMdijitali on Monday, April 25, 2022 | April 25, 2022
SERIKALI YAWEKA MPANGO MKAKATI
MAALUM WA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI
YA MALARIA NCHINI
Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI imeweka mpango mkakati maalum wa miaka mitano kuanzia 2021-2025 unaolenga kupunguza kiwango cha maambukizi ya Malaria.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kilele cha
maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ambayo yameadhimishwa kitaifa
jijini Dodoma.
Waziri Ummy amesema mpango Mkakati huo unalenga
kupunguza kiwango cha maambukizi ya Malaria nchini kutoka wastani wa
asilimia 7.5 ya mwaka 2017 hadi kufikia wastani wa chini ya asilimia 3.5
ifikapo mwaka 2025.
“Mpango huu una mikakati mikuu mitatu ambayo ni udhibiti wa mbu waenezao Malaria, uchunguzi, tiba na tibakinga ya Malaria kwa makundi maalum; na ufuatiliaji na tathmini ya mwenendo wa ugonjwa wa Malaria hapa nchini”. Amesema Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema katika kipindi cha mwaka 2021 jumla ya vyandarua milioni 7.5 vyenye dawa vimegawiwa kwa wananchi kupitia kliniki za wajawazito na watoto, shule za msingi za Umma na kupitia kampeni maalum ya usambazaji na ugawaji wa vyandarua katika kaya.
Aidha, Waziri Ummy ameongeza kuwa zaidi ya nyumba 568,000 zimepuliziwa viuatilifu ukoko kwenye kuta ndani ya nyumba na hivyo kuwakinga zaidi ya watu milioni 2 dhidi ya maambukizi ya Malaria katika Halmashauri za Kakonko, Kasulu na Kibondo pamoja na Kambi za wakimbizi za Nduta, Mtendeli na Nyarugusu kwa Mkoa wa Kigoma; Halmashauri ya Biharamulo kwa Mkoa wa Kagera; Halmashauri ya Ukerewe kwa Mkoa wa Mwanza na Halmashauri ya Bukombe kwa Mkoa wa Geita.
Waziri Ummy ameongeza kuwa Serikali imeendelea kununua na kusambaza vitendanishi na dawa za kutosha za kutibu Malaria katika vituo vya kutolea huduma za afya, ambapo vipimo na matibabu ya Malaria yanatolewa kwa wananchi bila malipo na upatikanaji wake ni asilimia 98.
Kwa upande wa upatikanaji wa dawa, Waziri Ummy amesema Serikali imekua ikifuatilia ubora na usalama wa dawa za Malaria na kujiridhisha kuwa ni salama na zina uwezo wa kutibu kwa zaidi ya asilimia 96.
Waziri Ummy amesema Serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kutekeleza afua mbalimbali za Malaria ambapo
KINANA ATEMA CHECHE ZIARANI MKOA WA PWANI
Written By CCMdijitali on Sunday, April 24, 2022 | April 24, 2022
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akipanda mti mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya CCM Tabi CCM Mwanambaya |
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana, akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mio wa Pwani, Ramadhani Maneno baada ya kuwasili patika ofisi za CCM Wilaya ya Mkuranga. |
Viongozi mbalimbali na wanachama wa CCM wakisimama kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM alipowasii katika ukumbi wa mkutano kwa ajili ya mkutano wa ndani wa Chama wilayani Mkranga. |