Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrhaman
Kinana amepata fursa ya kuelezwa masuala mbalimbali atakayoanza nayo
baada ya kupitishwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho
wakiongozwa na Mwenyekiti wao Rais Samia Suluhu Hassan.
Kinana
amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi upande wa
Tanzania Bara baada ya kupitishwa kwa kura zote 1875 ambazo zimepigwa na
wajumbe wa mkutano huo waliokutana leo Aprili 1,2022 Mjini Dodoma.
Akizungumza
mbele ya wajumbe hao wa Mkutano Mkuu wakiongozwa na Rais Samia, Kinana
amesema kwamba kabla ya jina lake kupelekwa Kamati Kuu na kisha
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, aliitwa na Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na walizungumza kwa saa mbili.
"Niilitwa
na Rais ,nikaenda na nilipofika nikamwambia niko tayari kwa kusikiliza,
mazungumzo yalichukua zaidi ya saa mbili,alinieleza mambo ya Chama,
alinieleza mambo ya Serikali.Nitajitahidi kufanya kazi ya Makamu
Mwenyekiti kwa bidii kwa lugha nyingine niseme sitakuangusha Mwenyekiti
wetu.
"Nawashukuru Kamati Kuu kwa kupitisha jina langu,
Halmashauri Kuu nashukuru lakini nawashukuru ninyi wajumbe wa mkutano
Mkuu kwa kunipa kura zote,.kunipa kura zote mmenitishwa mzigo, mmenipa
imani na imani huzaa amani.Pia shukrani zangu nazipeleka kwa Makamu
Mwenyekiti wa Chama chetu mzee Mangula.
"Mimi ni mwanafunzi wa
mzee Mangula akiwa Chuo cha Kivukoni nilikuwa mwanafunzi wake , nimekuwa
na Mangula kwenye vikao vya Chama, akiwa Makamu Mwenyekiti kiti wa CCM
mimi nilikuwa Katibu Mkuu.Nakushukuru kwa mafunzo na maelekezo yako
kwangu,"amesema Kinana.
Aidha Kinana amesema anawashukuru
viongozi wote ambao amefanya nao kazi tangu Awamu ya kwanza hadi Awamu
ya Sita inayoongozwa na Rais Samia na kwamba sifa zote zimetokana na
viongozi hao na mapungufu aliyonayo ni yake mwenyewe
Kuhusu kazi
atakayoanza k nafasi hiyo amesema kwanza atahakikisha Chama
kinaendelea kuwa imara,kinachokubalika na ili kiwe imara lazima
demokrasia iwe imara lazima wasimamie haki."Haki hiyo iwe ni haki ya
kuchagua,haki ya kuchaguliwa bila upendeleo,bila rushwa,bila umaarufu.
"Haki
ya pili ni ya kutoa mawazo, lazima wanachama wawe huru kutoa
mawazo,hakuna haki miliki ya kutoa mawazo, hivyo tutamsikiliza kila
mwanachama,kila mwananchi, hata kama maamuzi yametolewa hukuyapenda
sikiliza kisha jenga hoja .Lazima tuheshimu demokrasia kama alichaguliwa
mtu na wanachama kwanini tumpinge, tuilinde haki ya kuchagua na
kuchaguliwa,
"Rais nimefuatilia mara nyingi sana akizungumzia
haki, hata wakati anapokea ripoti ya mkaguzi mkuu akizungumza
haki.Lazima tuwe mfano wa kusimamia haki na kukataa dhuluma,"amesema
Kinana.
Aidha amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zote zinatokana na CCM,
hivyo CCM si mali ya Serikalini ila serikali hizo ni za CCM.Hivyo CCM
haipokei maagizo kutoka Serikalini ila CCM inaagiza Serikali kupitia
Ilani na ahadi za wagombea wake na hata wanaokwenda kugombea ni CCM sio
Serikali.
"Hivyo Serikali msitunyang'anye hiyo haki ya kusimamia
Ilani,sera na ahadi, Serikali inapofanya vizuri na kupewa sifa, wana CCM
wanayo nafasi ya kusifia na pale Serikali inapokosea wana CCM wanayo
haki ya kukosa lakini kwa kutumia vikao.
"Kwa hiyo kwa maoni
yangu Mzee Mkapa alisema semeni CCM pale mambo mbalimbali
yanapotekelezwa na bahati mbaya siku hizi haisemwi CCM , hivyo ni wajibu
wa CCM kusema yanayofanywa na tuisimamie Serikali na leo nimesoma
mabadiliko ya Katiba inasema kutakuwa na vikao kila baada ya miezi
sita,hapo ndipo itakuwa sehemu ya kutathimini utekelezaji wa Ilani
"Chama
hili kina historia, Chama hiki kinakubalika upende usipende,lazima
tuhakikishe Chama kinabakia kuwa sikio,Chama hiki kitembelee wananchi
kwenye maeneo yao, tuwe sikio lao, tukifanya hivyo wataendelea
kutuchagua,"amefafanua Kinana.
Ameongeza kuwa atatekeleza
majukumu yake kwa mujibu wa Katiba inayoeleza wazi atafanya kazi kwa
maelekezo ya Mwenyekiti wa Chama hivyo hata akifanya ziara kwa
wanananchi katika maeneo mbalimbali wajue atakua amepata baraka za
Mwenyekiti wake.
Pamoja na hayo,Kinana amemshukuru Mwenyekiti wa
Chama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini na nafasi
hiyo inafanya kuingia kwenye utamaduni wa viongozi wengine waliowahi
kuwa Makatibu Wakuu wa Chama na baadae kuwa Makamu Mwenyekiti.
Mbali
ya shukrani,Kinana amezungumzia umuhimu wa Umoja ndani ya Chama hicho
ambacho ni kikubwa na kinapendwa na kwamba CCM haina haina mwenyewe bali
ni ya watu wote, haina Ukanda.
"Nitasimamia hilo,mtu akikosa
hoja,akikosa maarifa anakimbilia kwenye kichaka cha ukanda, ukabila na
udini.Huo sio utamaduni wa Chama hiki, tunaweza kutofautiana kwa hoja
lakini sio kwa kuleta mambo ukanda,"amesisitiza.
Home »
KITAIFA
» HOTUBA YA KINANA KWA WAJUMBE MKUTANO MKUU MAALUM CCM YAWA GUMZO, ATAJA ATAKAYOANZA NAYO
HOTUBA YA KINANA KWA WAJUMBE MKUTANO MKUU MAALUM CCM YAWA GUMZO, ATAJA ATAKAYOANZA NAYO
Written By CCMdijitali on Friday, April 1, 2022 | April 01, 2022
Labels:
KITAIFA