Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Mohamed Mchengerwa |
MAAFISA MICHEZO SIMAMIENI VIKUNDI VYA MAZOEZI- MCHENGERWA
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Mohamed Mchengerwa @mmchengerwa
amewaagiza Maafisa Michezo nchini, kuvisajili vikundi vyote vya mbio
za hisani (Marathon) katika wilaya zao na kuvifuatilia ili kutoa motisha
kwa vikundi vinavyofanya vizuri na kuwaandaa wanariadha kushiriki
mashindano ya kimataifa na kusaidia kuzuia maradhi mbalimbali.
Mhe,
Mchengerwa ametoa agizo hilo leo, Aprili 10, 2022 wakati akizungumza na
Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mbio za
hisani kwa ajili ya utoaji wa elimu na ufahamu kuhusu usonji zilizo
andaliwa na taasisi ya Usonji ya Lukiza.
Ameongeza kuwa
wanariadha hao bora watakaopatikana kupitia mbio mbalimbali watashiriki
mashindano ya kimataifa na kuliletea taifa medali mbalimbali.
Akizungumzia
mashindano ya Jumuiya ya madola, Waziri Mchengerwa amesema washiriki
wote watakao kwenda kushiriki katika michezo hiyo Serikali inawahudumia,
na wote wapo kambini wakiendelea kujiandaa vyema kuwakabili washindani
wao katika mashindano hayo.
“Sisi kama Serikali tumeamua kwamba
wachezaji wetu watakaa kambini kwa takribani miezi kwa gharama ili
wapate maaandalizi bora ya kiwango cha kimataifa. Mategemeo yetu ni
kwamba warudi na medali za ushindi na ninasisitiza katika kipindi changu
hakuna wacheza kwenda kutalii bali kushiriki mashindano na kushinda”
amefafanua Mhe, Mchengerwa.
Ametoa wito kwa Watanzania wenye
uwezo wa kufundisha michezo mbalimbali kujitokeza kutokana na uhaba wa
makocha wa michezo hapa nchini.
“Hatuna makocha kabisa tukianzia
kwenye Mpira wa Miguu na michezo mingine kwahiyo tuna kazi kubwa kama
Wizara kwenda kuwandaa watanzania ili tuweze kupata makocha wa kutosha.”
Amesema Mhe, Mchengerwa.
Mbio hizo zilikuwa zimegawanyika katika
makundi matatu ya Kilometa 21, Kilometa 10 na kilometa 5 na
kuwashirikisha zaidi ya wanariadha 800. @cloudsfmtz @michuzijr @millardayo @tbc_online @habarileo_tz @dodoma_zone_ @dodoma_zone_ @officialmataga @timesfmtz @efmtanzania @ortamisemi