Balozi wa India hapa Nchini Mhe.
Binaya Pradhan akiongea |
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul |
MHE GEKUL- TANGAZENI UTAMADUNI WA TANZANIA
Serikali
kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imewataka watanzania
wanaopata fursa za masomo nje ya nchi kuitumia fursa hiyo vyema
kuzitangaza tamaduni za Tanzania huko ughaibuni.
Rai hiyo
imetolewa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Pauline Gekul wakati wa
maadhimisho ya siku ya Utamaduni wa Baraza la Mahusiano ya Kitamaduni la
India (ICCR) iliyoadhimishwa Aprili 09, 2022 katika ubalozi wa India
hapa nchini.
Katika maadhimisho hayo yaliyowakutanisha zaidi ya
wahitimu 50 walionufaika na fursa za udhamini wa masomo ya elimu ya juu
nchini India Mhe. Gekul amesema Serikali inawategemea sana watanzania
wanaopata fursa za udhamini wa masomo nje ya nchi kuwa mabalozi wa
utamaduni wa nchi yao.
“Mimi ninaamini mnapokuwa huko ughaibuni hamuishii tu kujifunza tamaduni za kwao, bali pia na nyinyi muwafundishe tamaduni zetu, na hasa lugha yetu ya Kiswahili”. Alisema Naibu Waziri Gekul .
Aliongeza kuwa “ tunategemea huko mliko mtakuwa mabalozi wazuri wa kuanzisha vituo vya utamaduni, na madarasa ya kufundishia lugha ya Kiswahili, ili hawa wenzetu wanaotupa ushirikiano na kutufadhili kwenye masomo waweze kujua lugha pamoja na tamaduni zetu”
Halikadhalika amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia na India zimekuwa na mahusiano ya karibu sana kwa miaka mingi sasa na kupitia udugu huo, nchi hizo zimekuwa zikishirikiana katika mambo mbalimbali hivyo, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Utamduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inaendelea na hatua za utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya Kiutamduni kati ya India na Tanzania ili nchi hizi mbili ziendelee kunufaika na programu ya ushirikiano katika masuala ya Kiutamaduni.
Kwa upande wake Balozi wa India hapa Nchini Mhe. Binaya Pradhan, Amesema tangu kuanza kwa kwa program hii ya ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa vijana wa Kitanzania zaidi ya watanzania mia tatu wamenufaika ambapo kwa msimu wa mwaka 2021 – 2022 watanzania 53 wamepata ufadhili katika ngazi za Shahada ya kwanza, Shahada ya Umahiri na Shahada ya Uzamivu.@officialpaulinegekul @tbc_online @michuzijr @millardayo @