WAWILI WASHIKIKIWA KWA TUHUMA ZA
KUGHUSHI NYARAKA
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili RAPHAEL STEVEN
(34) mfanyabiashara na mkazi wa Uyole Jijini Mbeya na PETER NATHAN (49)
mfanyabiashara na mkazi wa Mwakibete Jijini Mbeya kwa tuhuma za
kughushi na kutumia mihuri ikiwemo ya uwakili kujipatia kipato isivyo
halali.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ULRICH MATEI amesema
kuwa watuhumiwa walikamatwa Aprili 4, 2022 huko maeneo ya sokoine jijini
Mbeya baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za siri.
Aidha
ameeleza kuwa, katika upekuzi watuhumiwa walikutwa na mhuri wa uwakili
unaomilikiwa na BENARD GWAKISA (35) Wakili wa kujitegemea na mkazi wa
Manga Veta.
Nyaraka nyingine walizokutwa nazo ni nyaraka za
mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), BRELA, leseni mbili za biashara kutoka
halmashauri ya Jiji la Dodoma, manispaa ya kinondoni na laini za simu.