Malkia wa
Uholanzi, Malkia Maxima amewasili Jijini Dar es Salaam akitokea mkoani
Kilimanjaro ambapo alianzia ziara yake jana tarehe 17 Oktoba 2022 baada
ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 17 –
19 Oktoba, 2022.
Mara
baada ya Malkia Maxima kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam, alipokelewa na Mkurugenzi wa
Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza.
Malkia
Maxima ambaye pia ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa katika masuala ya Mfumo Jumuishi wa Fedha katika Maendeleo
anatarajia kukutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 19 Oktoba 2022.
Mbali
na kukutana na Mhe. Rais Samia pia Malkia Maxima kabla ya kuhitimisha
ziara yake hapa nchini, anatarajia pia kukutana na viongozi mbalimbali
waandamizi wa Serikali.
|
Malkia wa Uholanzi, Malkia Maxima akipokelewa
na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert
Kahendaguza baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam |
|
Malkia wa Uholanzi, Malkia Maxima akiwasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es
Salaam. Pembeni yake mwenye suti ya kijivu ni Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza |
|
Malkia wa Uholanzi, Malkia Maxima akimueleza jambo
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza
baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) Jijini Dar es Salaam |
|
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Robert Kahendaguza akiteta jambo na Malkia
wa Uholanzi, Malkia Maxima baada ya Malkia kuwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam |