Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wampa mapokezi makubwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan uwanja wa CCM Lake Tanganyika.
Mapenzi haya makubwa kwa Rais Samia yanahusishwa na jitihada zake kupitia Serikali anayoiongoza ya kuifanya Mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha biashara ukanda wa Magharibi.
Serikali ya awamu ya sita anayoiongoza Rais Samia inakamilisha ujenzi wa barabara za lami zinazouunganisha Mkoa wa Kigoma na Mikoa ya Tabora, Kagera na Katavi.
Inatekeleza pia miradi ya ujenzi wa meli kubwa mbili kwa ajili ya abiria na mizigo, inakamilisha ujenzi wa bandari ya Ujiji na Kibirizi, inakamilisha ukarabati wa meli ya kubeba mafuta ya MT Sangara, imeuunganisha Mkoa huo na umeme wa Gridi ya Taifa pamoja na uimarishaji mkubwa wa hospitali ya rufaa ya Mkoa huo Maweni.
Hakika wanakigoma #Tunaridhika #HakunaKilichosimama #KaziIendelee