Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mh Hashimu Mgandilwa Oktoba 18, 2023 amezindua zoezi la ugawaji bure wa Miche ya mikonge kwa wakulima ndani ya Jiji la Tanga zoezi ambalo limefanyika katika kitalu cha Miche ya Mkonge kilichopo katika kata ya Pongwe.
Akizungumza wakati wa kugawa Miche hiyo Mh. Mgandilwa amewataka wakulima kuitumia Miche hiyo ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuotesha vitalu binafsi vya Miche ya mkonge jambo litakalowasaidia kujikwamua kiuchumi.
Awali akitoa taarifa ya kitalu hicho Afisa Kilimo na Umwagiliajo wa Halmshauri ya Jiji la Tanga Hawa Msuya amesema kitalu kina jumla ya miche laki tatu na elfu hamsini na tano ambapo jumla ya wakulima 96 kutoka kata kumi za Jiji la Tanga watanufaika kwa kupata miche hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Sporah Liana amesema licha ya kuvuna miche na kugawa kwa wakulima upo mpango wa kukiendeleza kitalu hicho kwa ajili ya kuzalisha miche ya mkonge kwa wingi zaidi.
Katika ziara hiyo Mh Mgandilwa ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kukagua eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Mzizima pamoja na ukaguzi wa ujenzi wa majengo katika kituo cha afya Tongoni
#tkfmhabari
@hashimmgandilwa
@wizara_ya_kilimo
@bashehussein
@ofisi_ya_dc_tanga
@ofisiyamkuuwamkoawatanga
@tanga_jiji
Imeandikwa na @clever_m2mweus