Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi Hospitali Rufaa ya Kanda - Chato kujengwa kama ilivyokusudiwa
Rais Samia ametoa ahadi hiyo leo katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda - Chato
"Hospitali hii mpaka sasa majengo matano yapo tayari Niwahakikishie tutaijenga kama ilivyokusudiwa, wataalamu wakutosha wamesha letwa na tutaendelea kuwaleta" Amesema Rais Samia
Aidha Rais Samia amewataka Wana Chato kujitokeza kwa wingi kujiunga na Bima ya Afya kwa wote pindi itakapoanza kufanya kazi ili kupata Huduma bora za afya katika Hospitali hiyo kwa gharama zilizo ndani ya Bima hiyo.
"Niwaombe sana tutakapo kuja na mfumo wa Bima ya Afya kwa wote, wote tukanunue bima ni kupitia bima hizo tunaweza tukaboresha zaidi huduma hizi za afya" Amesema Rais Samia @samia_suluhu_hassan #kaziiendelee