Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema barabara kuu ya Kutoka Dar es salaam kuelekea Mpakani Tunduma imelemewa.
Akizungumza katika ziara yake Mkoa wa Songwe Mbarawa amesema ufinyu wa barabara hiyo unaweza kuwa chanzo cha Mlundikano wa magari katika mpaka wa Tunduma .
"nimekuja kuangalia hali halisi ya mpaka kiufupi barabara hii ya mpaka imelewa, na tayari serikali imeshaandaa mkakati wa kutatua Changamoto hii tayari makampun nane yameshajitokeza kwaajili ya Ujenzi wa barabara hizi nne, Rais samia ameshaliona tatizo hili ndiyo maana ametoa fedha za Ujenzi wa barabara hizo nne" amesema Mbarawa.
Aidha Mbarawa amezungumzia upungufu wa mashine ya scana katika upande wa nnchi jirani hali ambayo inachangia kuwepo kwa mlundikano wa magari mpakani hapo .
Hata hivyo Mbarawa ametembelea mipaka yote miwili katika Mkoa wa Songwe ambapo amekagua daraja lililopo Mpaka wa Malawi,lakini pia Mbarawa ametembela Mpaka wa Tunduma na baadaye kuendelea Mkoani Rukwa .