Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu ametembelea kituo cha kutibu magonjwa ya mlipuko na ambukizi cha Temeke {Temeke Isolation Center} pamoja na Kipawa kujionea utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola.
Waziri Ummy amesema kuwa Ugonjwa wa Ebola ni tishio huku hadi kufikia jana katika nchi ya Uganda ambapo kuna ugonjwa wa Ebola wamepata wagonjwa wapya 5 na kufanya idadi ya waliopata maambukizi hayo tangu mlipuko {Septemba, 2022} kufikia sasa ni jumla ya watu 126.
Amesema waliolazwa {Active Cases Admitted in hospital} 54 na vifo 32 vimethibitika. Uganda kufikia sasa wanafuatilia watu 2183 {contacts} ambao walikuwa karibu na watu waliothibitishwa kuwa na ebola.
"Wasiwasi wetu unazidi baada ya kuwa ugonjwa umeingia Kampala na Entebbe kwa hiyo ndege zinazokuja kutoka Kampala, kuja Dar es Salaam na mabasi "Kuibuka kwa Ebola Uganda kunaiweka Tanzania katika hatari ya kupata mlipuko huu Kutokana na mwingiliano mkubwa wa kiuchumi na kijamii na Uganda" amesema Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha Waziri Ummy amesema timu ya wataalam ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko itapatiwa mafunzo ya namna ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola ili waweze kutoa huduma bora.