SHIMIWI kufunguliwa rasmi, lakini Ikulu, Bunge zavutwa
Na Mwandishi Wetu, Tanga
WAKATI michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), itafunguliwa rasmi Jumatano Oktoba 5, 2022 kwenye uwanja wa Mkwakwani, baadhi ya timu za mihimili ya Serikali ikiwemo Ofisi ya Rais Ikulu na Ofisi ya Bunge zimeshindwa kufurukuta kwenye michezo yake ya kuvuta kamba wanaume kwa kuvutwa na wapinzani wao katika uwanja wa shule ya sekondari ya Usagara.
Michuano hiyo iliyoanza Oktoba 2, 2022 kwenye viwanja mbalimbali jijini hapa itafunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
Hata hivyo, katika michezo iliyofanyika ya miamba timu ya Ofisi ya Rais Ikulu wamevutwa na Idara ya Mahakama kwa mivuto 2-0; wakati timu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) waliwavuta Ofisi ya Bunge kwa mivuto 2-0; huku timu nyingine zilizoshinda kwa mivuto 2-0 kwa wanaume Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) waliwavuta Wizara ya Katiba na Sheria; nao Wizara ya Maliasili na waliwavuta ndugu zao Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo; na Wizara ya Elimu waliwavuta Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi).
Katika michezo mingine timu zilizoshinda ni Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari waliwavuta Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma; huku Wizara ya Mambo ya Ndani waliwavuta Ofisi ya Waziri Mkuu Sera kwa 2-0; nao Wizara ya Kilimo waliwavuta Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum; Hazina waliwavuta Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ; huku Tume ya Haki za Binandamu na Utawala Bora waliwavuta RAS Singida; RAS Kigoma waliwavuta Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; nazo Wizara ya Maji walitoka sare na Ukaguzi 1-1; na timu zilizopata ushindi wa chee ni Wizara ya Mambo ya Nje baada ya RAS Manyara kutoingfia uwanjani.
Kwa upande wa wanawake timu zilizoshinda kwa mivuto 2-0 ni Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) waliwavuta Ofisi ya Bunge; huku RAS Simiyu waliwavuta Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi; nayo Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara waliwavutaRAS Sindida; huku Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serkali za Mitaa (TAMISEMI) waliwavuta Bohari ya Dawa; nao Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki waliwavuta RAS Shinyanga; nayo Wizara ya Elimu waliwavuta RAS Mbeya; wakati Wizara ya Afya walitoka sare na Hazina kwa mvuto 1-1.
Timu zilizopata ushindi wa chee baada ya wapinzani wao kuingia mitini ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) dhidi ya RAS Ruvuma; nayo Idara ya Mahakama dhidui ya RAS Manyara; na RAS Iringa dhidi ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Katika mchezo wa netiboli uliochezwa uwanja wa Bandari , Timu ya Ofisi ya Rais Ikulu imewafunga RAS Dar es Salaam kwa magoli 60-8, nayo Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imewachapa RAS Mbeya magoli 19-7, huku Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepata ushindi wa magoli 40 baada ya timu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutokufika uwanjani; wakati Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wameibuka kidedea dhidi ya Tume ya Utumishi wa Walimu kwa magoli 30-10; na katika uwanja wa Polisi Chumbageni timu ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) waliwafunga ndugu zao Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa magoli 38-5.
Katika mchezo wa soka uliochezwa katika uwanja wa Shule ya Sekondari Popatlal Wizara ya Afya waliwapiga bila huruma RAS Dar es Salaam kwa magoli 4-0; wakati Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) wamewafunga RAS Lindi kwa magoli 4-0; huku katika uwanja wa Shule ya Sekondari Galanos timu ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi) imewafunga Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa goli 1-0;. Wakati huo huo, timu ya Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewafunga Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa 1-0.
MWISHO