Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) wamekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kutokana na tabia yake ya kupinga mambo mbali mbali yanayofanywa na Serikali hata kama yana manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Rais wa Jumuiya hiyo Ndg. Frank Nkinda amesema kwa kipindi kirefu, Chama hicho kimejijengea tabia Mbaya_ya kutafuta uungwaji mkono hata katika masuala yasiyo na maslahi kwa Taifa na kupinga mapendekezo yenye dhamira ya kuwaweka watanzania pamoja.
Akitolea mfano wa baadhi ya mambo hayo ikiwemo ripoti ya kikosi kazi iliyokabidhiwa juzi kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa imesheheni mapendekezo mbali mbali yenye tija kwa taifa letu. *Nkinda alisema wao kama wasomi wa Elimu ya juu hawaoni sababu yeyote ya Chadema kuipinga ripoti hiyo*
“Sote tulisikia muhtasari wa kile kilichowasilishwa na Mwenyekiti wa Kikosi kazi, Prof. Rwekaza Mukandala kwa Mhe. Rais, kwakweli dhamira yake ni njema. Sasa tumeshangaa kakikundi kamoja kamekuja juu na kusema mapendekezo haya hayafai na kwamba ni matumizi mabaya ya fedha za umma, _lakini ikumbukwe kwamba watu hawa waliitwa kutoa maoni yao wakakataa, sasa wanataka hata yale yaliyotolewa na watanzania wengine kwa uhuru na haki watu wayapinge_ ”alisema Nkinda
Aliongeza kuwa TAHLISO kama Taasisi inayolea nguvu kazi ya Taifa, kimsingi wana mamlaka ya Kuonya, kukemea na kushauri mambo mbalimbali katika Kuchochea maendeleo ya Taifa.
" Tumesikitishwa na kauli ya Katibu mkuu wa Chadema John Mnyika ya kuita ripoti hiyo kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuwa tu wao walikataa kuwasilisha maoni kwenye kikosi kazi cha Rais" alisema Nkinda
Alisema mtu au taasisi yoyote ya kiungwana ilipaswa kupongeza dhamira iliyoonyeshwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kutafuta maridhiano ya kitaifa kwa kupata maoni ya wadau juu ya njia gani za kupita kabla ya kufikia hitimisho na siyo kulalamika mbele ya vyombo vya habari suala alilosema halina msingi wowote.
Aliongeza kuwa Watanzania wameipokea ripoti hiyo kwa mikono miwili na wanawapongeza wadau wote walioshiriki kutoa maoni kwenye kikos...