Na Shamimu Nyaki
Timu
ya Taifa ya Wanawake chini ya Miaka 17 ( Serengeti Girls), inatarajia
kucheza na Colombia katika robo fainali baada ya kuandika historia kwa
mara kwanza kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia baada ya
kuitoa timu ya nchini Canada.
Mechi ya Robo Fainali baina ya Tanzania ( Serengeti Girls) na Colombia itachezwa Oktoba 22, jijini Goa India.
Katika
mchezo na Canada, Serengeti Girls ilikua inahitaji kushinda sare ya
aina yoyote, katika mechi hatimaye ilifanikiwa kupata sare ya goli 1 -
1.
Naibu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul ameongoza
Watanzania kuishangilia na kutoa hamasa ya kutosha kwa timu hiyo, ambapo
amesema Tanzania sasa inatangazwa vyema kupitia Sekta ya michezo.
Akizungumza
mara baada ya mchezo kumalizika, Mhe Gekul ameishukuru Serikali chini
ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha timu hiyo ya Serengeti
kuanzia kuweka Kambi ya kutosha katika Mji wa Southampton nchini
Uingereza ambapo ilifanya maandalizi mazuri ambayo yameifikisha hapo
timu hiyo.
"Nawapongeza sana wanangu hawa, wameliheshimisha Taifa, wameitangaza Tanzania, sasa hivi sio Royal Tour peke ake inayoweza kuitangaza nchi yetu bali hata Sekta ya michezo imeiweka Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye vipaji na kujulikana zaidi" amesema Mhe. Gekul.
Kwa
upande wa Kocha Bakari Shime, amesema Wasichana wamefanya vizuri baada
ya kufuata maelekezo aliyowapatia pamoja na kurekenisha makosa
waliyoyaona katika mechi zao mbili za kwanza, huku akisema Wasichana hao
siku zote wana ari ya ushindi na wamekua na utulivu kiakili pamoja na
nidhamu ya hali ya juu.
Tanzania
Sasa inaungana na Japan katika kundi D kutinga hatua ya robo fainali,
baada ya
Ufaransa na kutoa sare na Canada na hatimaye kupata
alama nne nyuma ya Japan wenye alama 9.kuifunga