Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi , Mhe. Caroline Kitana Chipeta, awasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi.
Hafla hiyo imefanyika katika moja ya Kasri za Kifalme iliyoko Noordeinde, The Hague, Uholanzi tarehe 19 Oktoba, 2022.
Julai 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alimteua Balozi Caroline Kitana Chipeta kuwa Balozi wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi, Mhe. Caroline Kitana Chipeta akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi |
Balozi wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi, Mhe. Caroline Kitana Chipeta katika picha na Mtukufu Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme huyo |
Balozi wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi, Mhe. Caroline Kitana Chipeta akizungumza na Mtukufu Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme huyo |