Home » » WAZIRI UMMY: BILION 11 KUJENGA JENGO LA MAMA NA MTOTO CHATO

WAZIRI UMMY: BILION 11 KUJENGA JENGO LA MAMA NA MTOTO CHATO

Written By CCMdijitali on Sunday, October 16, 2022 | October 16, 2022

Na. WAF – GEITA

Waziri wa Afya, Mhe. @ummymwalimu amesema kuwa serikali itatumia kiasi cha shilingi Bilioni 11 kujenga Jengo la mama na Mtoto Chato ndani ya mwaka wa Fedha 2022/2023.

Waziri @ummymwalimu amebainisha hayo kwenye Mkutano wa Hadhara Mkoani Geita wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mkoani humo.

Akizungumza Mhe. @ummymwalimu amesema kuwa watahakikisha wanajenga hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato inakamilika kwa kuwa na huduma zote za kibingwa, ubingwa bobezi, magonjwa ya moyo, saratani, magonjwa ya ndani, magonjwa ya afya ya mama na mtoto huduma hizo zinapatikana ndani ya mkoa wa Geita.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan nitahakikisha naweka kambi Mkoani Geita ili ujenzi wa hospitali ya rufa ya mkoa huu inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Geita na kuachia hospitali ilokuwa ya mkoa kuhudumu kama hospitali ya Halmashauri kusaidia kupunguza gharama kwa wananchi kufata huduma umbali mrefu”, ameeleza Waziri @ummymwalimu 

Kwa kuongezea Mhe. @ummymwalimu amesema kuwa sambamba na ujenzi wa vituo vya afya,hospitali za wilaya Pamoja na hospitali za rufaa za mikoa, vifaa tiba na watumishi watahakikisha huduma zinazotolewa ni huduma bora na sio bora huduma.

Hivyo ametoa wito kwa watumishi wa afya kuwa hudumia wananchi wote kwa usawa kwa kuzingatia viapo vyao na maadili ya utoaji huduma za afya.

Aidha Waziri @ummymwalimu amewataka watanzania kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa Ebola uliopo nchi ya Jirani Uganda kwa kuzingatia usafi binafsi na usafi wa afya kwa kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka nasabuni.

Vile vile amesisitiza kuwa king ani bora kuliko tiba hivyo kutokana na tishio la Ebola katika nchi Jirani ya Uganda na kipindu pindu katika nchi ya Malawi ni vema wananchi mkajihadhari kwa kuzingatia usafi.

Mhe. @ummymwalimu ameendelea kutoa rai kwa wale ambao bado hawajapata chanjo dhidi ya Uviko 19 kujitokeza kupata chanjo hiyo.

MWISHO








Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link