Home » » BYABATO :  RAIS SAMIA KUTOA ZAIDI YA BILIONI KUMI KUMALIZA TATIZO LA UMEME BUKOBA MANISPAA

BYABATO :  RAIS SAMIA KUTOA ZAIDI YA BILIONI KUMI KUMALIZA TATIZO LA UMEME BUKOBA MANISPAA

Written By CCMdijitali on Tuesday, November 1, 2022 | November 01, 2022

BYABATO :  RAIS SAMIA KUTOA ZAIDI YA BILIONI KUMI KUMALIZA TATIZO LA UMEME BUKOBA MANISPAA 

Naibu Waziri wa Nishati  na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Mhe. Stephen Byabato amesema kuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekubali kuleta zaidi ya bilioni kumi katika jimbo la Bukoba Mjini ili kukamilisha miradi ya umeme. 

Byabato aliyasema hayo wakati wa Ziara yake ya kutembelea kata 4 za Greenbelt na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025, kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa  jimboni hilo kuanzia  tarehe 27 Oktoba, 2022 na kumalizika 30 Oktoba, 2022. 

Aidha amesema awali Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alitoa bilioni 1.7 ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza tatizo la umeme katika Manispa ya Bukoba na kazi iliyobaki ni kuuganisha umeme kwenye nyumba. 

“Mimi wakati napewa nafasi ya kuwawakirisha katika ubunge mitaa minane haikuwa na umeme na sasa hakuna mtaa hata mmoja ambao hauna umeme" 

Pamoja na hayo wananchi wa Jimbo la Bukoba mjini wamemshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Mbunge wao namna ambavyo ameendelea kumimina maendeleo katika sekta zote ikiwemo maji, umeme, Afya na miundombinu ya Barabara. 

#ZiaraJimboni
#BukobaMpya
#KaziIendelee
@jimbo_bukoba_mjini
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link