Home » » Mheshimiwa Mgandilwa  na Kamati ya Usalama Wilaya wafanya ziara ya kutembelea viwanda vya saruji Wilayani Tanga.

Mheshimiwa Mgandilwa  na Kamati ya Usalama Wilaya wafanya ziara ya kutembelea viwanda vya saruji Wilayani Tanga.

Written By CCMdijitali on Thursday, November 24, 2022 | November 24, 2022



TANGA MJINI

Mkuu wa wilaya ya Tanga Mheshimiwa Hashim Mgandilwa  Novemba 24, 2022 akiambatana na Kamati ya Usalama Wilaya walifanya ziara ya kutembelea viwanda vya saruji kwa lengo la kukagua utekelezaji wa uthibiti uchafuzi wa mazingira hasa kutokana na uzalishaji wa saruji katika viwanda hivyo.

Mh Mgandilwa amewasisitizia wamiliki wa viwanda kuhakikisha wanaweka mifumo bora ya kuzuia kusambaa kwa vumbi,katika makazi ya Wananchi ili kupunguza athari za kiafya zitakazo jitokeza hapo baadaye kwa wale watako pata madhara kutokana na vumbi linalozalishwa katika viwanda hivyo ikiwa ni pamoja na kuandaa (Action plan) ya namna ya kutunza mazingira kwa kupanda miti mingi na mingine kugawa kwa wananchi.





@ofisi_ya_dc_tanga @ofisiyamkuuwamkoawatanga @hashimmgandilwa @dashian__
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link