TAREHE 07 NOVEMBA 2022 MKUU WA MKOA WA NJOMBE ALIENDESHA KIKAO KAZI MAALUM KWA WATENDAJI NA VIONGOZI KWAAJILI YA KUIMARISHA NA KUIKUZA WILAYA YA NJOMBE.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka, amewataka Watumishi na Viongozi kufanya kazi kwa weledi na kujituma ili kumsadia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Hayo ameyasema leo Novemba 7, 2022, katika kikao kilichofanyika Halmashauri ya Mji Njombe ambapo wajumbe walikuwa ni Mkuu wa Wilaya, Kamati za Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya, Waheshimiwa Wenyeviti wa Halmashauri na Madiwani, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara na Vitengo (CMT), Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji kutoka Halmashauri zote tatu zinazounda Wilaya ya Njombe, yaani Halmashauri Wilaya ya Njombe, Halmashauri ya Mji Njombe na Makambako.
Mhe. Anthony Mtaka amewataka wahusika kufanya kazi kwa weledi na kujituma katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo suala la ukusanyaji wa mapato kwani Mkoa wa Njombe unautajiri mkubwa hivyo Wataalamu wanauwezo mkubwa wa kubuni Vyanzo vingine vipya ili kuweza kuongeza na kukuza zaidi mapato katika Halmashauri zao.
Aidha Mhe. Mtaka amezungumzia suala la namna ya kuweza kukabiliana na janga la moto na utunzaji wa Mazingira
"Janga la moto katika suala la kuunguza misitu limekuwa ni tishio kwa uchumi wa Mkoa wa Njombe kwa kuwa kuanzia mwaka 2020 hadi 2022 misitu yenye thamani ya fedha ya Kitanzania zaidi ya shilingi Bilioni 316 imeungua". Alisema Mhe. Mtaka.
Mhe. Mtaka ameeleza kwamba majanga ya moto katika Mkoa wa Njombe yamekuwa yakisababisha misitu kuungua wakati misitu hiyo ndiyo msingi na chanzo kikubwa cha mapato.
amewasisitiza wenyeviti na watendaji kuwaelimisha wananchi lakini pia hatua stahiki ziendelee kuchukuliwa hasa katika kipindi hiki ambacho wanaandaa mashamba.
Katika kuboresha utendaji Vijijini Mhe. Mtaka amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuanza kuwalipa posho Wenyeviti wa Vijiji kwa kuwa wanasaidia sana suala la uhamasishaji wa maendeleo, utekelezaji wa miradi na usimamizi wa ukusanyaji wa mapato.
@samia_suluhu_hassan
@ikulu_mawasiliano
@angellah_kairuki
@ortamisemi
@nbs.tanzania @anthony_mtaka
@dc_njombe
@sharifa_nabal
@msemajimkuuwaserikal