Mh.Mkuu wa Mkoa, amesisitiza kuwa, lengo la kikao hiki ni kutafuta namna bora ya kutatua changamoto zote zinazokabili mpango wa ruzuku ya mbolea kwa mwaka 2022/2023.
Mh.Mkuu wa Mkoa, ameelekeza kuwa, Viongozi wa Serikali kutoka Ofisini na kwenda kuwatembelea wakulima na kusikiliza changamoto zao na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo.
Aidh, amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuchukua hatua za mara kwa mara kusikiliza kero za wakulima na kuzitatua kwa kuwasiliana na Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania ili kupata taarifa sahihi .