CPA MAKALLA: CCM ITAWALETEA WAGOMBEA WASIO NA MAKANDOKANDO

  Na Richard Mwaikenda, Mwanza   Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla akiwaahidi wananchi kwa...

Latest Post

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia katika Kilele cha Tamasha la Kizimkazi, Paje Zanzibar

Written By CCMdijitali on Thursday, August 31, 2023 | August 31, 2023

 Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia katika Kilele cha Tamasha la Kizimkazi, Paje Zanzibar

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Viongozi pamoja na Wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini wakati wa Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Paje, Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Viongozi pamoja na Wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini wakati wa Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Paje, Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Viongozi pamoja na Wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini wakati wa Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Paje, Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.

Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakipita kwa Maandamano mbele ya Jukwaa Kuu katika kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Paje Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.

Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakipita kwa Maandamano mbele ya Jukwaa Kuu katika kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Paje Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.



Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Paje kwa ajili ya kuhudhuria Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.

Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Paje kwa ajili ya kuhudhuria Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.

Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Paje kwa ajili ya kuhudhuria Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.

Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Paje kwa ajili ya kuhudhuria Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.


Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Paje kwa ajili ya kuhudhuria Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.

Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Paje kwa ajili ya kuhudhuria Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.

Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Paje kwa ajili ya kuhudhuria Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.

Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Paje kwa ajili ya kuhudhuria Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.

Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Paje kwa ajili ya kuhudhuria Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Zanzibar tarehe 31 Agosti, 2023.

WIZARA YA ARDHI YAJA NA MABADILIKO MAKUBWA YA KIMFUMO

WIZARA YA ARDHI YAJA NA MABADILIKO MAKUBWA YA KIMFUMO

Na Munir Shemweta, WANMM, 
BAGAMOYO

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema inaendelea kufanya maboresho makubwa ya kimfumo na muundo kwa lengo la kuewezesha mambo mengi ya wizara hiyo kufanyika  kimfumo,

Hayo yamebainishwa leo tarehe 31 Agosti 2023 na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga wakati akizindua zoezi la kuondoa mlundikanao wa mashauri katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, uzinduzi uliofanyika wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Amesema, kumekuwa na changamoto kubwa hasa wananchi wa kawaida wanapokwenda ofisi za ardhi kupata namba ya malipo (Control number) hivyo wizara inakuja na mfumo utakaomuwezesha mwananchi kupata namba hiyo ya malipo mwenyewe.

’Kumekuwa na changamoto kubwa hasa wananchi wetu wa kawaida wanapokwenda ofisi zetu za ardhi kupata tu control namba inakuwa changamoto, inakuwa kama ni deal sasa tunakuja na mfumo utakaomuwezesha mwananchi kupata control number mwenyewe’’ alisema Eng Sanga

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, hata suala la kufanya search kwa wananchi wanaotaka kununua nyumba au kiwanja nalo anaweza kufanya mwenyewe ambapo kwa sasa analazimika kutoa fedha ili kufanyiwa.

‘’Mnafahamu mtu akitaka kununua nyumba au kiwanja cha mtu katika kufanya upekuzi anaambiwa pia alipe shilingi elfu arobaini au laki moja afanyiwe haraka haraka nayo pia tunaenda kukomesha, mwananchi atafanya upekuzi mwenyewe’’ alisema Eng. Sanga

Aliongeza kwa kusema, kubwa zaidi katika maboresho hayo ni suala la kulipia kodi ya pango la ardhi ambapo kazi yake inakwenda kukamilika hivi karibuni ambapo wananchi wataweza kulipia kupitia simu ya mkononi sambamba na kupata bili kama wanavyopata katika maji.

‘’Utakapokuwa na namba ya NIDA utapata mambo yote,  katika wizara yetu ya ardhi wamelizingatia agizo la Mhe. Rais ambapo kwa kutumia kitambulisho cha NIDA mwananchi atapata taarifa zote kuhusina na masuala ya ardhi’’ alisema Eng Sanga.

Akigeukia zoezi la kuondoa mlundikano wa mashauri ya ardhi, amesema zoezi hilo ambalo uzinduzi wake umefanyika pia kwenye wilaya za Musoma, Tarime, Ifakara pamoja na Tabora katika kipindi  cha mwezi mmoja jumla ya mashauri 500 yanatarajiwa kusikilizwa na kutolewa maamuzi.

‘’Katika kipindi takriban siku nane toka kuanza kwa zoezi hili wenyeviti wameweza kusikiliza mashauri 243 katika Mabaraza niliyoyataja ambalo zoezi hilo linaendeshwa’’ alisema Eng Sanga.

Kwa upande wake Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya nchini Stela Tullo ameishukuru Wizara ya Ardhi kupitia Mradi wa Uboreshaji Miliki za Ardhi kwa kuyawezesha Mabaraza kuhakikisha yale yanayoelemewa na migogoro angalau yanapata msaada wa wenyeviti kwenda kwenye mabaraza yenye mashauri mengi na kuyakalia vikao maalum kwa lengo la kusikilizwa na kutolewa maamuzi kwa wakati na haki.

---------------------------------------MWISHO--------------------------------------------

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga akizungumza wakati wa akizindua zoezi la kuondoa mlundikanao wa mashauri ya ardhi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya katika wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani tarehe 31 Agosti 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga akizindua zoezi la kuondoa mlundikanao wa mashauri ya ardhi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, uzinduzi uliofanyika wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani tarehe 31 Agosti 2023.

Sehemu ya washiriki wa uzinduzi wa zoezi la kuondoa mlundikanao wa mashauri ya ardhi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya uliofanyika Bagamoyo mkoa wa Pwani tarehe 31 Agosti 2023.

Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Stela Tullo akizungumza kwenye uzinduzi wa zoezi la kuondoa mlundikanao wa mashauri ya ardhi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya uliofanyika wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani tarehe 31 Agosti 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga akisikiliza moja ya shauri katika Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Bagamoyo mara baada ya kuzindua zoezi la kuondoa mlundikanao wa mashauri ya ardhi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya tarehe 31 Agosti 2023.

Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Nyumba na Wilaya wilaya ya Kibaha na Bagamoyo Mhe. Mathias Lung’wecha akiendesha shauri la ardhi lililohudhuriwa na Katibu Mkuu wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga. Wengine katika picha ni Wazee wa Baraza.

Baadhi ya Wadaawa wakioongozwa na Wakili wakiwa katika usikilizwaji shauri la ardhi katika Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Bagamoyo tarehe 31 Agosti 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)




HEINEKEN KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KUKUZA VIPAJI NCHINI

Written By CCMdijitali on Wednesday, August 30, 2023 | August 30, 2023

HEINEKEN KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KUKUZA VIPAJI NCHINI

Katibu Mkuu wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa masuala ya ushirikiano kimataifa kutoka kampuni ya vinywaji vya Heineken Bw. Frank Ford ambapo wamejadiliana namna bora ya kushirikiana na kuendeleza Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kikao cha viongozi hao kimefanyika Agosti 30, 2023 katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana kutumia matukio ya Michezo na Sanaa katika kuwahudumia wananchi kupitia matamasha, mikutano mbalimbali, tuzo za michezo, tuzo za filamu, tuzo za muziki pamoja na uibuaji na uendelezaji wa vipaji vya michezo na Sanaa.

Katibu Mkuu Yakubu amesema Wizara ipo mstari wa mbele kuhakikisha sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo zinapata ufadhili kutoka kwa makampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuendeleza vipaji vya Sanaa na michezo nchini.

Kwa upande wake Bw. Frank Ford ameupongeza uongozi wa Wizara kwa kazi nzuri inayofanya kuendeleza sanaa na michezo nchini na kuahidi kampuni yake itaendelea kushirikiana na Wizara katika kuendeleza sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ahudhuria Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) kwenye Tamasha la Kizimkazi, Paje Zanzibar



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika viwanja vya Paje kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) Paje Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea Jukwaa Kuu kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) Paje Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vikundi mbalimbali vya Sanaa vikitumbuiza kwenye Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) katika viwanja vya Paje Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023.

Viongozi, Wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwa kwenye viwanja vya Paje kuhudhuria Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) lililofanyika Paje Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023.

Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Simba wakati akikagua mabanda mbalimbali yaliyopo kwenye viwanja vya Paje katika Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023.



KATIBU MKUU BW. YAKUBU AKUTANA NA VIONGOZI WA BENDI YA MLIMANI PARK

KATIBU MKUU BW. YAKUBU AKUTANA NA VIONGOZI WA BENDI YA MLIMANI PARK

Katibu Mkuu wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na kikundi cha bendi ya Mlimani Park, kuhusu kushirikiana na wizara katika matukio mbalimbali ya Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kikao hicho kimefanyika Agosti 30, 2023 katika ofisi za wizara zilizopo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana namna bora kikundi hicho cha muziki wa densi kinaweza kutumika kuelimisha jamii kupitia muziki huo katika matamasha mbalimbali nchini.

ZIARA YA MAKAMU WA PILI JIMBO LA ZIWANI NA WAWI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema uhai wa Chama Cha Mapinduzi ni wanachama walio hai hivyo, amewataka Viongozi wa CCM kuhakikisha Idadi ya wanachma wanaojiunga na CCM inazidi kuongezeka.

 

Ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Wanachama wa CCM na Wananchi wa Jimbo la Ziwani na Jimbo la Wawi ambapo amesema ni vyema kuwa na takwimu sahihi za Wanachama ambazo zitatumika kupata Idadi sahihi ya wapiga Kura ambao watakivusha Chama ifikapo mwaka 2025

Mhe. Hemed ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa Ilani ya CCM inaendelea kutekeleza Ilani kwa kujenga miradi mbali mbali ya maendeleo hivyo, amewataka Wananchi kutoe mashirikiano kwa Serikali ili kuweza kukamilisha miradi hiyo.

Aidha amewapongeza Wananchi wa Ndagoni waliotoa maeneo yao ya kilimo kwa kupisha Mradi wa ujenzi wa Barabara maamuzi ambayo yanaonesha utayari wa Wananchi kuungana na Serikali yao katika ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo.

Amewataka Wananchi kuendelea kuziunga Mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt.  Hussen Ali Mwinyi na kuwahakikishia kuwa miradi yote iliyotajwa katika Ilani na ile iliyoelekezwa na Rais  inatekelezwa kwa faida ya wazanzibari.

 

Amefahamisha kuwa mkakati wa Serikali ya Awamu ya Nane inayoongzwa na Dkt Hussen Ali Mwinyi ni kuhakikisha wanawawezesha Vijana na Wanawake kupitia miradi mbali mbali ya kuwawezesha wananchi kiuchumi ili nao waweze kunufaika na matunda ya CCM na Serikali kwa ujumla.       

 

Aidha amewataka Wananchi wa Majimbo hayo kuendelea kuishi kwa Amani na Upendo ambao ndio msingi wa maendeleo na kuwataka wapenda maendeleo kuiunga mkono CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amewataka Viongozi wa CCM kwa Ngazi zote kuchangamkia fursa mbali mbali na kuzielekeza kwa Vijana wanaojitolea katika Chama ili kujipatia kipato na kupungua ukali wa maisha.

 

Nae Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chakechake Ndg. Ali Muhamed Chande ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kulinda Amani na utulivu uliopo hatua ambayo imepelekea kwa kiasi kikubwa kuweza kufikia maendeleo iliyojipangia.

 

Amewataka wananchi kuendelea kuungana na Serikali katika kuilinda Amani na utulivu ili kuweza kurahisisha kufanyika kwa shughuli mbali mbali za kijamii.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mhe. Dkt. Abdallah Rashid ameeleza kuwa Serikali kupitia dhana ya uchumi wa buluu imejenga kiwanda cha kuanikia Dagaa eneo la Ndagoni hatua ambayo itawasadia waanika dagaa kuweza kufanya shughuli zao bila ya changamoto zozote.

Katika ziara hiyo Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amepokea Taarifa za utekelezaji wa Majimbo hayo na kukagua ujenzi wa Matawi na Maskani kwa lengo la kuimarisha Chama na Jumuiya zake.

 

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

30 Agosti, 2023

 
 
 

 


WAZIRI MABULA AKUTANA NA MKURUGENZI WA TAASISI YA RRI

Written By CCMdijitali on Tuesday, August 29, 2023 | August 29, 2023



Na Munir Shemweta, WANMM

 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo yavMakazi Mhe. Dkt Angeline Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali  kutoka Marekani Bw. Patrick Kipalu.

 

Dkt Mabula amekutana na mkurugenzi huyo anayeshughulika na Programu za Haki na jitihada za Rasilimali Ardhi katika Bara la Afrika katika ofisi ya Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma tarehe 29 Agosti 2023.

 

Mazungumzo ya viongozi hao mbali na mambo mengine yamelenga maandalizi ya Kongamano la Nne la Kimataifa litakalofanyika jijini Arusha kuanzia 12- 15 Sept 2023 likiwa na  agenda kuu ya upatikanaji wa hatimilki za ardhi.

 

Taasisi hiyo ya Marekani ndiyo wadhamaini wa kongamano hilo linalojadili masuala mbalimbali yahusuyo masuala ya ardhi ikiwemo hati milki za ardhi.

 

--------------------mwisho------------------------

 


 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali  kutoka Marekani Bw. Patrick Kipalu jijini Dodoma tarehe 29 Oktoba 2023.

 

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasilimali  kutoka Marekani Patrick Kipalu (katikati) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardhi Imaculata Senje jijini Dodoma tarehe 29 OKtoba 2023.

 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali kutoka Marekani Patrick Kipalu jijini Dodoma tarehe 29 Oktoba 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)


Rais Samia aweka jiwe la msingi Ujenzi wa Soko la CRDB Kizimkazi Dimbani, Kusini Unguja Zanzibar

Rais Samia aweka jiwe la msingi Ujenzi wa Soko la CRDB Kizimkazi Dimbani, Kusini Unguja Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan
(watatu kushoto) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya CRDB Bank
Foundation, Martin Warioba (kushoto) wakifanya tukio la uzinduzi wa
ujenzi wa soko la kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani linalojengwa kwa
ufadhili wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu
takribani Shilingi Bilioni Mbili hadi kukamilika kwake. Hafla hiyo
ambayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la
Kizimkazi, imefanyika leo Agosti 29, 2023, Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan
(watatu kushoto) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya CRDB Bank Foundation, Martin Warioba (kushoto) wakifanya tukio la uzinduzi wa ujenzi wa soko la kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani linalojengwa kwa
ufadhili wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu
takribani Shilingi Bilioni Mbili hadi kukamilika kwake. Hafla hiyo ambayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi, imefanyika leo Agosti 29, 2023, Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan
 (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi
ya CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa kuhusu ujenzi wa soko la
kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani linalojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu takribani Shilingi Bilioni Mbili hadi kukamilika kwake. Hafla hiyo
ambayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la
Kizimkazi, imefanyika leo Agosti 29, 2023, Kizimkazi mkoa wa Kusini
Unguja, Zanzibar. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Abdulmajid Nsekela.



Kizimkazi, Zanzibar, 29 Agosti 2023: Katika juhudi za kuendelea kuwezesha jamii inayoizunguka kupitia sera yake ya uwekezaji kwa jamii, Benki ya CRDB kupitia Tasisi yake ya CRDB Bank Foundation inatarajia kujenga soko la kisasa katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja visiwani Zanzibar. Hafla ya kuweka jiwe la msingi la soko hilo imefanyika katika eneo la Kizimkazi Dimbani kama sehemu ya shamra shamra za tamasha la Kizimkazi na kuhududhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko hilo, Rais Dkt. Samia ameishukuru Benki ya CRDB kwa kukubali ombi la Mkoa wa Kusini kujenga soko hilo la kisasa ambalo litachochea maendeleo ya watu wa Kizimkazi na Mkoa wa Kusini Unguja kwa ujumla.


“Mwaka jana kama mnakumbuka mlinipa kilio hiki cha soko la jamii ya Kizimkazi. Sasa mimi nikalitupa Mkoa ambapo na wao wakalipeleka CRDB na leo wako hapa kwenye field tayari kuweka jiwe la msingi na ujenzi unaendelea. Kwa hiyo tuwashukuru sana CRDB kwa kutushika mkono katika hilo na haya ndo maendeleo ya Kusini tuliyoyasema na ndo madhumuni ya tamasha letu hili la Kizimkazi” alisema Rais Dkt. Samia.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kwa kutambua uchumi wa watu wa kusini unatemegea sana uvuvi, Benki chini ya Taasisi yake ya CRDB Bank Foundation imeamua kuwekeza katika ujenzi wa soko la kisasa ambalo litakwenda kuongeza thamani katika biashara kwa wakazi wa eneo la Kizimkazi. Katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa soko, Benki imetenga takribani Shilingi Milioni 157.8 na tayari ujenzi wa sehemu ya kwanza tayari umeanza.


“Kwa muda mrefu Benki ya CRDB imekua mdau mkubwa wa maendeleo ya Kizimkazi kupitia tamasha la Kizimkazi ambapo hadi kufikia tamasha la mwaka huu, Benki ya CRDB imeshafanya uwekezaji wa takribani Shilingi Bilioni 1 na soko hili la kisasa la Samaki litaghrarimu zaidi ya Bilioni 2 hadi kukamilika kwake ambapo sehemu ya kwanza ya ujenzi itakamilika mnamo mwezi Oktoba 2023” amesema Nsekela.



Mbali na utoaji wa huduma za fedha kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano, Benk ya CRDB pia imekua ikitekeleza sera yake ya uwekezaji katika jamii katika pande zote mbili. Sera hiyo ya uwekezaji katika jamii inaelekeza 1% ya faida kurejeshwa katika jamii katika maeneo ya elimu, afya, mazingira na uwezeshaji kwa wanawake na vijana.

Mbali na ujenzi wa soko hili la kisasa, Benki kupitia taasisi yake ya CRDB Bank Foundation imeendelea na dhamira yake ya kuleta mageuzi katika mchezo wa Resi za Ngalawa ambapo katika tamasha la Kizimkazi la mwaka 2023, Benki imewekeza zaidi ya Milioni 119.5 katika mashindano ya Resi za Ngalawa ambazo ni sehemu ya Tamasha la Kizimkazi” aliongeza Nsekela.



Mwaka 2021, Benki ya CRDB ilikua mdhamini kuu wa Tamasha la Kizimkazi kwa kugharamia tamasha lote asilimia kuanzia mafunzo kwa wajasiriamali, michezo, maonyesho ya wafanyabiashara hadi kilele cha tamasha. Mbali na hilo Benki ilifadhili ujenzi wa nyumba za madaktari na Ofisi ya Sheha.

Mwaka 2022, Benki ya CRDB ilijenga maabara ya Shule ya Sekondari ya Kizimkazi pamoja na kununua vifaa vyake vya maabara. Sambamba na hilo Benki ilifadhili michezo yote na zaidi kuleta mapinduzi katika mchezo wa Resi za Ngalawa ambapo uliweza kuvutia watu wengi zaidi na kutoa zawadi kubwa zilizoweza kubadili maisha ya wana Kizimkazi ikiwemo zawadi kubwa ya boti ya kisasa yenye thamani ya Shilingi Milioni 30 kwa mshindi.

 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link