Mkuu wa wilaya Kilindi Mh Hashim Mgandilwa amelishukuru shirika lisilo la kiserikali World Vision ADP Mgera kwa kufadhili Mradi wa maji utakaonufaisha wakazi wa Kijiji cha Ngobore kilichopo kata ya Saunyi
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Mradi huo tarehe 28/08/2023 Mh Mgandilwa alisema ili Mradi huo iendelee kuwepo na kunufaisha walengwa kwa muda mrefu ni lazima miundombinu yake itunzwe vizuri
Alisema serikali inayoongozwa na Dk Samia Suluhu Hassan imekuwa ikitafuta fedha kwa ajili ya miradi ya maji pamoja na kushirikiana na wadau wa Maendeleo ili kutatua kero ya maji
Awali akitoa taarifa ya Mradi huo mratibu wa ADP Mgera Modest Kessy alisema Mradi huo ulioanza mwaka 2022/2023 na umegharimu shilingi milioni 259,279,000/= na unategemea kunufaisha watu 2801 wanawake wakiwa 884,wanaume 847 na watoto 1076 na kuishukuru serikali kwa ushirikiano mkubwa katika kipindi chote cha utekelezaji Mradi
Modi Mngumi
Mawasiliano Serikalini Kilindi DC
@ofisiyamkuuwamkoawatanga
@ccm_kilindi @waziriwazirik @ortamisemi