Taasisi ya Jamii Mpya Mkoa wa Tanga tarehe 26/8/2023 wameandaa Kongamano la kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anazofanya katika kuongoza nchi na kutekeleza miradi mingi ya maeneo nchi nzima ikiwemo katika Mkoa wa Tanga.
Mhe Ummy amewapongeza Jamii Mpya Mkoa wa Tanga kwa wazo lao zuri la kumpongeza na kumtia moyo Rais wetu Dkt Samia kwa kuwa ni kweli Kazi za Rais Samia katika nchi hii ni kazi kubwa, kazi nzuri na kazi zinaonekana kila mkoa, kila Wilaya, kila Kata na Kila Kijiji na Mtaa yote nchini.
Mhe Ummy ameendelea kusema kuwa Kazi za Rais Samia zinaonekana kwenye sekta za Elimu, Afya, Maji, Nishati, Miundombinu ya barabara, Kilimo na Uvuvi. Hivyo tunapaswa kumpongeza, kumtia moyo na kumuunga mkono ili aendelee kuwatumikia vyema watanzania.
Akiwasilisha Hotuba yao kwa Mgeni Rasmi, Katibu wa Jamii Mpya mkoa wa Tanga Bi. Halima Bughe amesema kuwa lengo la Jamii Mpya ni kumpigania Rais Samia sambamba na kuibua na kuzisemea kero za wananchi hasa wanawake, watoto na vijana. Hivyo wameona waandae kongamano hilo ili kumpongeza Rais sambamba na kuzindua Rasmi Taasisi ya Jamii Mpya Mkoa wa Tanga ambayo tayari wana wanachama zaidi ya 2,000 katika Wilaya za Tanga Mjini, Muheza, Korogwe, Mkinga, Pangani, na Kilindi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na mratibu wa Jamii Mpya Tanzania ndg. Ally Makwiro, Mratibu wa Jamii Mpya Mkoa wa Tanga Mwalimu Mwajuma Selemani, Katibu wa CCM wilaya Tanga ndg. Seleman Sankwa, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Abdurahaman Shiloo waheshimiwa madiwani na viongozi wengine wa chama na serikali na wanachama wa jamii mpya kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Tanga.
Imetolewa na;
Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Tanga Mjini.
27/08/2023.