Home » » "Kesi yeyote ya ardhi itakayoonekana watendaji katika serikali au wenyeviti wa vijiji wanahusika wahusika hao watafikishwa mahakamani kwa majina yao na sio taasisi"- DC Kilindi, Tanga

"Kesi yeyote ya ardhi itakayoonekana watendaji katika serikali au wenyeviti wa vijiji wanahusika wahusika hao watafikishwa mahakamani kwa majina yao na sio taasisi"- DC Kilindi, Tanga

Written By CCMdijitali on Monday, August 28, 2023 | August 28, 2023


Mkuu wa wilaya Kilindi Mh Hashim Mgandilwa amesema kuanzia Sasa kesi yeyote ya ardhi itakayoonekana watendaji katika serikali au wenyeviti wa vijiji wanahusika wahusika hao watafikishwa mahakamani kwa majina yao na sio taasisi

Mh Mgandilwa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa tarafa za Mgera,Mswaki na viongozi wa kisiasa katika tarafa hizo kilichofanyika katika kata ya Kwediboma

Alisema ifike wakati tuone kila uhai una thamani kubwa na wanaotumia migogoro ya ardhi kwa manufaa yao hawatavumiliwa tena kwani migogoro ya ardhi na mingine katika Wilaya imekuwa ni tatizo ambalo kila mmoja anapaswa kuhakikisha tatizo hilo linaisha ama kupungua ili masuala mengine ya maendeleo yaendelee

Mh Mgandilwa alisema ikitokea mgogoro Kama vile mfugaji ameingiza mifugo katika shamba la mtu na kesi hiyo ikaripotiwa sehemu husika na baadae mkulima atoe taarifa ya kukataa kuendelea na shauri hilo kwa maamuzi wamemalizana wenyewe mkulima au mhusika huyo aliyesema haendelei na shauri hilo atafikishwa yeye mahakamani

Alisema hatua hiyo itatekelezwa kwa sababu ya kukithiri migogoro ya ardhi katika Wilaya Kilindi

Kikao hicho kilishirikisha waheshimiwa madiwani,wenyeviti wa vijiji na watumishi wa tarafa za Mgera na Mswaki

Mawasiliano Serikalini Kilindi DC


@ofisiyamkuuwamkoawatanga 
@ccm_kilindi @waziriwazirik @ortamisemi
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link