Na Eleuteri Mangi, WUSM, Tanga
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu ametoa wito kwa makampuni mbalimbali ndani na nje ya Tanzania kujitokeza kudhadhili vilabu vya soka na michezo mbalimbali nchini ili ziwe na ushindani katika medani za kitaifa na kimataifa.
Katibu Mkuu Bw. Yakubu ametoa wito huo jijini Tanga akiwa Mgeni Rasmi wakati timu ya Coastal Union ilpokuwq ikisaini mkataba na kampuni ya Elsewedy Electric Cable East Africa Ltd ambayo itaifadhili timu hiyo kwa msimu wa 2023/2024 pamoja na kuzindua jezi itakayotumika kwa msimu huu.
"Mpira sasa unahitaji vitu vitatu, ufundi kwa maana ya utaalam wa michezo kwa wachezaji na viongozi, vipaji vya wachezaji vinavyokuzwa na kulelewa na kuwaandaa kuwa wachezaji bora ambao watumiwa na vilabu, timu ya taifa na hata soka la kulipwa nje ya nchi pamoja na fedha ambazo ndiyo chachu ya soka na michezo mingine kwa kuzingatia michezo ni ajira" amesema Katibu Mkuu Bw. Yakubu.
Amewataka uongozi wa timu ya Coastal Union kutumia fedha zitakazotolewa na wafadhili hao kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuweka mikakati mizuri ya ushindi.
Aidha, ametoa wito kwa Mfadhili huyo Mpya na kusisitiza kuwa Coastal Union ni dude lililolala, ufadhili wao na utaalam utaiamsha timu hiyo ili ifanye vizuri katika medani ya soka kwa kuzingatia Misri ni taifa kubwa kisoka barani Afrika na kuwataka waisaidie timu hiyo kupate wasaa wa kuwa na maandalizi mazuri ya msimu ujao kwa kuwapa nafasi ya kuweka kambi nchini Misri.
Kwa upande wao Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Elsewedy Electric East Africa Mhandisi Ibrahim Qamar na
Mkurugenzi wa Biashara katika Miradi Bw. Muhammad El Shazly wamesema wanafuraha kufanyakazi na timu ya Coastal Union kwa kuwa historia zao zinafanana, kampuni hiyo imeanzishwa mwaka 1938 na timu ya Coastal Union imeanzishwa 1948.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa timu hiyo Steven Mguto amesema ufadhili ambao wamepata utasidia timu hiyo kutekeleza majukumu yake ya msingi ambayo ni kuijenga timu iwe na ushindani na kushika nafasi nne za juu katika ligi ya NBC ili mwakani washiriki mashindano ya kimataifa.
Timu ya Coastal Union imeanzishwa mwaka 1948 na imewahi kuwa bingwa mwaka 1988 huku wachezaji nguli kuchezea timu hiyo na timu ya Taifa. Wachezaji hao ni Mohamed Mwameja, Ally Maumba, Yasin Napili, Idrisa Ngulungu, Mohammed Salum, Hilal Hemed, Mchunga Bakari, Riffat Saidi, Juma Mgunda, Bakari Mwanyeto na Abdalah Sopu.
Home »
MICHEZO NA BURUDANI
» MAKAMPUNI JITOKEZENI KUFADHILI VILABU VYA SOKA NCHINI
MAKAMPUNI JITOKEZENI KUFADHILI VILABU VYA SOKA NCHINI
Written By CCMdijitali on Sunday, September 17, 2023 | September 17, 2023
Labels:
MICHEZO NA BURUDANI