Home » » RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BANDARI YA SAMAKI KILWA NA KUGAWA BOTI 160 KWA WAVUVI.

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BANDARI YA SAMAKI KILWA NA KUGAWA BOTI 160 KWA WAVUVI.

Written By CCMdijitali on Tuesday, September 19, 2023 | September 19, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega pamoja na viongozi wengine wakati akiweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko Mkoani Lindi tarehe 19 Septemba, 2023.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack, Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuzindua ugawaji wa Boti za Uvuvi 34 za mkopo nafuu mara baada ya kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi, Kilwa Masoko Mkoani Lindi tarehe 19 Septemba, 2023.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega mara baada ya kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi tarehe 19 Septemba, 2023. View all comments

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan leo September 19 ameweka Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa pamoja na kugawa wa Boti 34 kati ya 160 zilizonunuliwa na Serikali kwa Wavuvi na Wakulima wa Mwani. Hayo yamejiri Wakati wa Ziara ya Kikazi Mkoani Lindi Wilaya ya Kilwa ambapo Rais Samia amesema Ujenzi wa Bandari hiyo utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 260 na itachukuwa muda wa miezi 36 kukamilika. 
 
Kuhusu Boti 34 kati 160 alizogawa kwa Wavuvi, Rais Dkt,Samia amesema boti hizo zinatolewa kwa mkopo nafuu na kuwataka Wavuvi waliokabidhiwa kurejesha mkopo kwa wakati. Hata hivyo *Rais Samia* amesema Serikali imekusudia kufufua mji wa Kilwa kiuchumi na kuurudisha kwenye hadhi yake kama zamani.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link