"Neema ya majiko ya gesi 140, mitungi 140 na meza 140 na kreti za soda 140 zawashukia Mama NTILIE"
Mbunge wa Tanga Mjini Mhe.Ummy Mwalimu leo tarehe 09/09/2023 amegawa majiko ya gesi 140, mitungi ya gesi 140 na meza 140 na kreti za soda 140 kwa wajasiliamali wanawake wanaojihisisha na biashara ya Chakula (Mama Lishe/Mama Ntilie) wa Jijini Tanga. Ambapo jumla ya wanawake wajasiriamali 480 watanufaika
Vifaa hivyo vilivyotolewa chini ya Kampeni ya Mwanamke Shujaa vimedhaminiwa na Kampuni ya Cocacola Kwanza na Oryx Gas Tanzania na vina thamani ya shilingi milioni thelathini na tano (35,000,000/-). Kampeni hiyo yenye Kauli mbiu ya Mwanamke Shujaa "Jiamini, Jithamini na Jijenge" pia imewashirikisha Taasisi ya Ustawi wa Jamii na TK FM Radio ya Tanga.
Mhe Ummy amewashukuru CocaCola na Oryx kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kuwawezesha wanawake. Aidha amewashukuru kwa kukubali ombi lake la kuja Tanga kuwajengea uwezo wanawake wa Tanga kuzitambua fursa za kiuchumi na kuwapatia vifaa hivi.
Hafla hiyo ya kukabidhi mitungi, majiko ya gesi na meza imehudhuriwa na Katibu Tawala Wilaya ya Tanga BiZ Dalimia Mikaya, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya jamii Coca-Cola Kwanza ndg Salum Nasoro, Mwakilishi wa Oryx Energies Tanzania Ndugu Shabani Fundi, Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Tanga ndg. Al Shaymaa Kwegyir, Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Tanga ndg. Moza Shilingi Mikaya, Waheshimiwa Madiwani wanawake, Kaimu Mkurugenzi Jiji la Tanga bi. Hawa Msuya na viongozi wengi na wajasiriamali.
Imetolewa na;
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Tanga Mjini
09/09/2023.
@cocacola_kwanza @ofisiyamkuuwamkoawatanga @mbungetangamjini @dashian__ @oryxenergiestanzania #TangaMjini #MahabaUkarimuNaMaendeleoZaidi #odoummyjimboni