Home » » UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI OLD MOSHI MAGHARIBI KATIKA TAMATI ZA KAMPENI.

UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI OLD MOSHI MAGHARIBI KATIKA TAMATI ZA KAMPENI.

Written By CCMdijitali on Tuesday, September 19, 2023 | September 19, 2023


JANA 18.09.2023 KISHINDO CHA KATIBU WA CCM MKOA/MNEC MABIHYA CHADHIHIRISHA USHINDI WA KISHINDO KWA CCM UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI OLD MOSHI MAGHARIBI KATIKA TAMATI ZA KAMPENI.

Wabunge @esthermalleko , Prof Patrick Ndakidemi &  @priscus4moshi wakoleza Chachu ya Ushindi katika Kata hiyo.

Moshi.

Chama Cha Mapinduzi kimefunga Kampeni zake za Ugombea wa Udiwani Kata ya Old Moshi Magharibi kwa kishindo katika maeneo ya Mande, ambapo Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro/Mnec Ndg. Jonathan Mabihya alikua Mgeni rasmi katika Mkutano huo Mkubwa wa Ufungaji wa Kampeni hizo.

Katika Mkutano huo Mhe. Mabihya alimkabidhi rasmi ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2020-2025 Mgombea wa Udiwani kwa tiketi ya CCM katika Kata hiyo Ndg. Peter Dustan Massawe ishara kuwa atakapoapishwa akatimize ahadi zake kulingana na Ilani hiyo ya CCM inavyosema kwani ndio Mkataba kati ya Watanzania na Serikali yao ya CCM.

Mabihya alisema "Kupitia CCM ni hakika kuwa Ndg. Peter Massawe ataweza kuwaletea maendeleo katika kata yenu lakini pia kupatikana ufumbuzi wa kero zinazowakabili na mahitaji yenu kwani kila kitu kimeainishwa vizuri katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025".

Mkutano huo ambao pia Ulihudhuriwa na Mbunge mwenyeji wa Jimbo hilo Mhe. Prof Patrick Ndakidemi akisindikizwa na Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Mhe. Priscus Tarimo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Esther Maleko ambao wote kwa pamoja walimuombea Kura Mgombea wa CCM kea wananchi wa Old Moshi Maghahribi.

Nae Mgombea wa Udiwani katika Kata hiyo Ndg. Peter Dustan Massawe aliwaomba wananchi hao kumchagua kuwa Diwani katika Kata hiyo huku akiwaeleza kuwa kwa kushirikiana na Mbunge na Rais Samia pamoja Viongozi wangu wa CCM tutafanikisha yote niliyoyahaidi huku akisisitiza kuwa yeye sio Mgeni katika Majukumu hayo kwani alishakuwa Diwani awali hivyo anazijua njia zote.

Mkutano huo Ulihudhuriwa pia na Afisa Idara ya Organaizesheni CCM Taifa Ndg. Jumanne Kitundu. Katibu wa CCM Wilaya Ndg. Ramadhani Mahanyu, Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi Ndg. Hussein Jamal, Mkt wa Wazazi CCM Mkoa Ndg. Daudi Babu Mrindoko, Mkt wa UWT Mkoa Ndg. Elizabeth Minde, Mjumbe wa Baraza Kuu

@ccmtanzania @mrindokomwidad











 

 

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link