Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Hashim Mgandilwa wa pili kulia akipata maelezo kutoka Kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Dkt. Mariam Ngwere (wa pili kulia) alipofanya ukaguzi wa Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
Katika ziara hiyo ya kukagua Miradi ndani ya kata ya Bokwa, Mafisa na Kibirashi Mhe. Mgandilwa aliambatana na Kamati ya Ulinzi (KU) Wilaya ya Kilindi.
Aidha Mhe. Mgandilwa amewataka watendaji wanaohusika na utekelezaji wa mradi wa Hospitali kufanya kazi Kwa bidii na kuepuka ucheleweshaji wa michakato yeyote itakayokwamisha ukamilishaji wa mradi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kusimamia fedha za Umma vizuri Kwa kufanya manunuzi Kwa gharama nafuu pale inapowezekana ili kuokoa fedha.
Lakini pia Amemtaka Mkurugenzi kuhakikisha hospital hiyo inazinduliwa rasmi ifikapo disemba mosi 2023 ili itoe huduma iliyokusudiwa kwa wananchi wa Kilindi.
Imetolewa na
Samwel Mwantona