Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amefanya ziara katika Chuo Kikuu cha Silk Road International University of Tourism and Cultural Heritage na kujionea mafunzo yanayotolewa na sambamba na nyenzo za kufundishia.
Akizungumza na Mkuu wa Idara ya Utalii katika chuo hicho leo Oktoba 20, 2023, Mhe. Kairuki ameeleza nia ya kuanzisha ushirikiano kati ya Chuo hicho na Vyuo vya Tanzania vinavyotoa mafunzo ya utalii na ukarimu.
Naye, Mkuu wa Idara ya Utalii wa Chuo hicho, Bw. Akmal Odilov alieleza kuwa ni Chuo cha kimataifa na chenye Wahadhiri wabobezi kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Aidha, aliongeza kuwa wako tayari kushirikiana na Tanzania katika kuboresha mitaala, kubadilisha wahadhiri sambamba na wanafunzi kutoka pande zote mbili.
Vilevile, alieleza kuwa Chuo hicho hutoa ufadhili wa Shahada ya Pili katika fani za Utalii na Ukarimu na watatoa kipaumbele kwa Tanzania.