Home » » Dc MSANDO AWASISITIZIA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA KUSOMA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI

Dc MSANDO AWASISITIZIA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA KUSOMA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI

Written By CCMdijitali on Friday, October 13, 2023 | October 13, 2023

MAAGIZO KWA WATENDAJI NA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA NA VIJIJI HALMASHAURI ZA WILAYA YA HANDENI, TANGA KUSOMA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI KWA ROBO YA KWANZA 2023/2024. 


Mkuu wa Wilaya ya Handeni Wakili Albert Msando anaendelea kuwakumbusha na kuwasisitizia wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji pamoja na Watendaji wao kuhakikisha wanawasomea mapato na matumizi wananchi wao kila baada ya miezi mitatu kama sheria na kanuni zilivyowaagiza. 

Kumekuwa na tabia baadhi ya wenyeviti na watendaji kwenye maeneo yao kushindwa kufanya hivyo watambue kuwa wanakiuka taratibu zao za kiutendaji .

 Aidha pia Mkuu wa Wilaya amewakumbusha wananchi wote kwamba wanapaswa kujitokeza na kushirki kwenye mikutano ya kusomewa mapato na matumizi. 

Wakurugenzi wote wa halmashauri za Wilaya na Mji Handeni wameagizwa kufuatilia na kusimamia zoezi hili kwa watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa.

 Mtendaji atakae shindwa kuwasomea wananchi mapato na matumizi atachukuliwe hatua kali za kiutumishi kwa uzembe na kutowajibika. 

Mwisho Mkuu wa Wilaya amewaelekeza wananchi wote kutoa taarifa endapo kutakuwa na ubadhirifu wowote wa mapato yao kwa Maafisa Tarafa na yatafanyiwa kazi kwa haraka.

 Imetolewa na; 

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Handeni, Tanga. 13/10/2023. 
Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link