Home » » DC NGORONGORO AKAGUA UJENZI SHULE YA SEKONDARI PINYINYI

DC NGORONGORO AKAGUA UJENZI SHULE YA SEKONDARI PINYINYI

Written By CCMdijitali on Friday, October 13, 2023 | October 13, 2023

 Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Raymond Mwangwala Leo tarehe 13 Octoba 2023 ametembelea Maendeleo ya Ujenzi wa  Shule mpya ya Sekondari PINYINYI

 Mhe.Mwangwala amesema Serikali inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Mwezi June 2023 kupitia mpango wa kuboresha elimu ya sekondari yaani SEQUIP ilileta sh. 584,280,028 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya SEQUIP kata ya Pinyinyi.


"Majengo yatakayojengwa ni ,Vyumba 8 vya madarasa,Jengo la utawala,Maabara 3 za sayansi,Jengo la TEHAMA ,Maktaba , Matundu 20 ya choo cha wanafunzi,Matanki ya kukusanyia maji" amesema Mwangwala

"Aidha Mwangalwa ameridhishwa na Ujenzi baadhi ya majengo na kuwataka  mafundi na wasimamizi Ujenzi Shule Hiyo kuongeza Kasi ya Ujenzi ili kukabuliana na Hali ya mvua  ya EL NINO inayotarajia kuanzia hivi Karibuni ili Ujenzi usisimame  na majengo yawe yamekamilika kabla ya tarehe  25 Octoba 2023


 




 

 

 

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link