ZIARA YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN MKOANI SINGIDA
SINGIDA
Waziri wa Ardhi Mhe Jerry Silaa amesema eneo la Sagara Wilaya ya Singida Mkoani Singida halina mgogoro wa ardhi baada ya mgogoro uliokuwepo eneo hilo kutatuliwa.
Waziri Silaa ametoa kauli hiyo tarehe 15 Oktoba 2023 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan alipopewa nafasi ya kusalimia wananchi wakati wa mwanzo wa ziara ya Rais ya siku tatu mkoani Singida.
" Nichukue fursa hii kumpongeza mkuu wa wilaya na Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Singida na viongozi wote wilaya hii, hapa Sagara hakuna mgogoro na ule uliokuwepo umekwisha na hali ya hapa ni shwari hakuna mabango" alisema Silaa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ameanza ziara yake ya siku tatu tarehe 15 Oktoba 2023 ambapo mbali na mambo mengine katika ziara yake atapokea taarifa ya mradi wa ujenzi wa shule zilizopokea fedha kupitia miradi ya BOOST, SEQUIP na Serikali Kuu, ataweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Mkiwa - Itigi - Noranga km 56.9 kwa kiwango cha lami pamoja na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha polisi Ikungi.
--------Mwisho----------








