Home » » RC MONGELLA AONGOZA HARAMBEE KANISA LA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI 

RC MONGELLA AONGOZA HARAMBEE KANISA LA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI 

Written By CCMdijitali on Sunday, October 15, 2023 | October 15, 2023



RC MONGELLA AONGOZA HARAMBEE KANISA LA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI USHARIKA TARAJALI WA MAGUNGANI JIJINI ARUSHA.


Mgeni rasmi na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella ameongoza harambee ili kupata fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa majengo matatu kwenye kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Ushatika wa Magungani ulioko kata ya Sokoni I Jiji la Arusha.

Akizungumza wakati wa kuongoza Harambee hiyo Mhe. Mongella ameushukuru uongozi wa kanisa kwa kumualika kufanya kazi hiyo ya kumtumikia Mungu, ambayo amethibithisha na kuahidi kushirikiana nao mpaka ujenzi huo utakapokamilika na u
Usharika huo tarajali utakapozinduliwa na kuwa Usharika kamili.

Amethibitisha kubarikiwa na kushibishwa na neno la Mungu lilohubiriwa lililowakumbusha waumini kujitoa na kuchangia kazi za Mungu na kuongeza kuwa yeye anaamini sadaka inayouma ndiyo sadaka ya kweli.

Aidha amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inatambu na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na madhehebu ya dini, kwa kutekeleza miradi mingi ya kuwahumiwa wananchi wa Tanzania, miradi ambayo kimsingi ingefanywa na serikali.

"Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anasisitiza viongozi wote wa serikali kushirikiana kwa karibu na makanisa na viongozi wa dini, kwa kuwa anathamini mchango unatolewa na Taasisi za dini kusadia jamii ya watanzania husani wenye kipato cha duni" Amesema Mhe. Mongella 

Hata hivyo changizo hilo limefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi milioni 13,218,500, ikiwa fedha taslimu milioni 7.4 na ahadi shilingi milioni 5.7 huku milioni 67.7 zikihitajika kufikia mwendo wa milioni 90 uliopangwa.

Katika harambee hiyo Mkuu huyo wa Mkoa kwa niaba ya ofisi yake amechangia kiasi shilingi milioni 5 kwa kutoa fedha taslimu shilingi milioni 1 na kuahidi kukamilisha shilingi milioni 4 kabla ya tarehe ya uzinduzi wa usharika huo mapema mwezi Novemba 2023

Akisoma risala ya  Harambe Mchungaji Kiongozi Usharika Tarajali wa Magungani, Mchungaji Thomas Kaika amesema lengo la harambee hiyo ni kukusanya shilingi milioni 90 kwa ajili ya kukamilisha jengo la utawala, darasa la shule ya Jumapili pamoja na maliwato za kisasa ili kuthibitishwa kuwa Usharika

#ARUSHAFURSALUKUKI🇹🇿 
#kaziinaendelea
 





 
















Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link