Nzega Vijijni-Tabora
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa shilingi Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Maji katika Kata ya Puge Wilaya ya Nzega, Mkoani Tabora.
Waziri wa Maji (Mb), Mhe. Jumaa Hamidu Aweso amemuhakikishia Mhe. Rais kuwa Wizara yake italeta Fedha hizo mapema iwezekanavyo ili kuwaondolea tatizo la maji wakazi wa Kata ya Puge.
Serikali inapeleka Fedha hizo za mradi wa maji Kata ya Puge kufuatia Ombi la Mbunge wa Nzega Vijijini Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala ambaye amesema ni kata moja tu ya Puge katika Jimbo lake ndio yenye changamoto ya uhaba wa maji.
Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora, ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake Mkoani humo.