RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA DKT. JOHN JINGU JIJINI DAR ES SALAAM
Swahili Caption Story
Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dr. John Jingu na ujumbe wake alipokutana nao ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Jumatano tarehe 18 Oktoba 2023.
Pamoja na mambo mengine, mazungumzo yao yalihusu zaidi maandalizi ya Mkutano wa Pili wa Kisayansi wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Kijana, na Lishe (RMNCAH+N) uliopangwa kufanyika tarehe 15-17 Novemba 2023.
Mkutano huo, unaoandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na washirika kadhaa ikiwa ni pamoja na JMKF, umepangwa kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julis Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam chini ya kauli mbiu: "Kukuza upatikanaji wa Huduma Bora za Uzazi, Mama na Mtoto, Kijana".
Makundi mbalimbali la wajumbe wa ndani na wa kimataifa wanatarajiwa kuhudhuria Mkutano huo ambao ulitokana na mikutano ya awali ya wadau wa RMNCAH.
Wazo la kufanyika kwa mkutano huo wa kila mwaka lilizaliwa katika moja ya mikutano ya kawaida ya kila robo ya Kikundi cha Kazi cha Kiufundi cha RMNCAH kwa lengo la kuleta wadau muhimu pamoja ili kusambaza, kuthibitisha, na kujifunza mafundisho yanayopatikana kwa vitendo bora na hatua za msingi zinazotokana na ushahidi ili kuzidisha utekelezaji.
Wizara ya Afya na washirika waliandaa mkutano wa kwanza kabisa wa RMNCAH mwezi Novemba 2021 katika ukumbi huo huo na ulifunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Zaidi ya wajumbe 1,400, wakiwemo wataalamu wa ndani na wa kimataifa walihudhuria.
Katie Mkutano wa Mwaka 2021, majadiliano makubwa yaliyotokana na mazungumzo katika vikao vidogo vidogo vilivyohusisha zaidi ya mawasilisho 200 yaliyolenga kuboresha mazingira wezeshi pamoja na upatikanaji wa huduma bora za RMNCAH + N nchini Tanzania.
Mwisho
English Caption Story
The Settlor and Chairman of the Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), retired President of the United Republic of Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, meets with the Permanent Secretary of the Ministry of Health Dr. John Jingu and his delegation today, Wednesday 18th October 2023, at his office in Dar es Salaam.
During the meeting, Dr. Kikwete and Dr. Jingu discussed a variety of issues, the majority of which concerned preparations for the upcoming 2nd Reproductive, Maternal, Newborn, Child Adolescent Health and Nutrition (RMNCAH+N) scientific Conference, which is set for November 15th - 17th, 2023 in Dar es Salaam.
The conference, coordinated by the Ministry of Health in partnership with numerous partners, including the JMKF, will take place at the JNICC in Dar es Salaam under the topic "Advancing access to quality reproductive, maternal, newborn, child, and adolescent health care."
The Conference, which came about from previously held annual RMNCAH stakeholders' meetings, is expected to draw a wide range of local and international participants.
The annual conference was conceived during one of the regular quarterly RMNCAH Technical Working group meetings in response to the need to bring key stakeholders together to disseminate, validate, and learn lessons from available best practises and evidence-based interventions for scale-up.
The Ministry of Health and partners hosted the first-ever RMNCAH conference in November 2021 at the same location, which was officiated by Hon Kassim Majaliwa, Prime Minister of the United Republic of Tanzania. Over 1,400 delegates attended, including dignitaries and local and international specialists.
Major topics from plenary and breakout sessions addressed almost 200 papers with the goal of enhancing the favourable environment, availability, and access to excellent RMNCAH + N services in Tanzania.
Ends