Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe.Tony Blair na ujumbe wake leo tarehe 05 Oktoba 2023 Ikulu Zanzibar.
Mazungumzo yao wamegusia fursa katika uchumi wa buluu ikiwemo sekta ya utalii wa fukwe, urithi ,michezo, mikutano , pamoja na uwekezaji, bandari, biashara, teknolojia, huduma za kijamii ikiwemo afya, elimu , na mafunzo ya kujenga uwezo.
Waziri Mkuu Tony Blair ameambatana na ujumbe wa Taasisi ya Tony Blair Institute(TBI).
🗓️05 Oktoba 2023
📍Ikulu, Zanzibar .