Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Huduma ya Afya kwa wote ni muhimu katika kufikia lengo la kutoa huduma bora za afya kwa kila mtanzania.
Serikali itahakikisha kuwa kila mwananchi bila kujali hali yake ya kifedha anapata fursa ya huduma za afya ya msingi.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 03 Oktoba 2023 akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa kumi wa Afya Tanzania(Tanzania Health Summit) uliofanyika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam pia amezindua Bodi ya wakurugenzi ya Tanzania Health Summit.
Vilevile Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali imeendelea kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya afya kwa kuongeza idadi ya vituo vya afya , hospitali katika bajeti ya maendeleo ya Serikali mwaka wa fedha 2023/24 jumla ya shilingi bilioni 203.47 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa hospitali za Wilaya, vituo vya afya na zahanati pia shilingi bilioni 116.9 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vya hospitali, vituo vya afya na zahanati pamoja kuongeza rasilimali watu.
🗓️03 Oktoba 2023
📍Ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.