Home » » RC MONGELA AUAGIZA UONGOZI WA JIJI LA KULIPA POSHO ZA WENYEKITI WA MITAA

RC MONGELA AUAGIZA UONGOZI WA JIJI LA KULIPA POSHO ZA WENYEKITI WA MITAA

Written By CCMdijitali on Wednesday, October 18, 2023 | October 18, 2023

RC AMEUAGIZA UONGOZI WA JIJI LA ARUSHA KULIPA POSHO ZA WENYEKITI WA MITAA KWA WAKATI; AWATAKA WENYEVITI KUSHIRIKI UKUSANYAJI WA MAPATO


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella kujipanga kulipa posho za wenyeviti wa vijiji kwa wakati kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Baraza la waheshimwa Madiwani.

Mhe. Mongella ametoa maagizo hayo mara baada ya kupokea malalamiko kutoka wa wenyeviti hao kwa halmashauri ya Jiji la Arusha kushindwa kuwalipa wenyeviti hao kwa muda sasa.

" Niwaelekeza Meya na Mkurugenzi na Baraza lenu la Madiwani, wekeni mipango ya kulipa fedha hizo kwa kuwa ni haki yao ya msingi kama yalivyokuwa makubaliano lakini zaidi yapo majukumu mengi wanayatekeleza ya kuwahudumia wananchi kwa niaba ya serikali"

Aidha amemtaka mkurugenzi huyo kujipanga kuwatumia wenyeviti hao kwa kushirikiana na Maafisa Watendaji wa kata  katika zoezi la ukusanyaji wa mapato kwa kuwa vyanzo hivyo vya mapato viko kwenye maeneo yao.

"Mkurugenzi andaa timu ya ukusanyaji wa mapato kuanzia ngazi ya kata kwa kuwa wanayo orodha ya baishara zote kwenye kata, wapeni 'training' waanze kazi ya kukusanya mapato, watalamu wa wilaya na halmashauri kuweni waratibu wa zoezi ili kufikia lengo la mwaka mlilojiwekea, kwa kuwa bado jiji lina asilimia ndogo kwa robo ya kwanza " Amesisitiza Mkuu huyo wa Mtaa.

Hata hivyo mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini, amekiri kuwepo kwa ucheleweshwaji wa kuwalipa wenyeviti hao kutokana na changamoto zilziojitokeza, changamoto ambazo tayari zimeshughulikwa na wataendelea kulipa fedha hizo kwa taratibu zilizowekwa.

Mhansisi Hamsini amekiri kupokea ushauri wa kuwatumia Watendaji wa kata na wenyeviti wa mtaa kukusanya mapato kwa makubaliano ya kuwalipa asilimia moja ya makusanyo yatakayopatika ili kuongeza kasi ya makusanya na kufikia lengo lililowekwa kwa mwaka.

"Kutokana na ukubwa wa jiji na idadi kubwa ya biashara, na idadi ndogo ya Maafisa Biashara, tutawatumia Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa kata kukusanya mapato katika maeneo yao"

 Amesema Mhandisi HamsiniKutokana na taratibu za Jiji la Arusha Wenyeviti wa serikali za Mitaa hulipwa posho ya shilingi 100,000 kwa mwezi.











Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link