Home » , » WAFANYABIASHARA WADOGO WATAKIWA KUKUBALIANA NA MABADILIKO - ARUSHA

WAFANYABIASHARA WADOGO WATAKIWA KUKUBALIANA NA MABADILIKO - ARUSHA

Written By CCMdijitali on Thursday, October 19, 2023 | October 19, 2023


WAFANYABIASHARA WADOGO WATAKIWA KUKUBALIANA NA MABADILIKO YANAYOTOKANA NA MAENDELEO YA KIUCHUMI.


Wafanyabiasha wadogo Jiji la Arusha, wametakiwa kukubaliana na mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea kwa kuwa ni mabadiliko yoyote lazima yanakuja na matokeo hasi ambayo huathiri sehemu na baadhi ya watu.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella wakati wa mkutano wa hadhara uliowakutanisha wafanyabiashara wa soko Kilombero, uliofanyika kwenye eneo la Sokoni hapo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo Jiji la Arusha.

Mhe. Mongela amesema hayo mara baada ya kusikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara hao wadogo waliolalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara za Jiji kwa baadhi ya maeneo, kuhamisishwa mara kwa mara, uchakavu wa soko hilo pamoja na  mpango wa kuhamishwa stendi ya Daladala eneo la Kilombero .

Akijibu kero hizo, Mhe. Mongella ameweka wazi mpango wa serikali ya awamu ya sita ni kutekeleza awamu ya pili ya mradi mkakati wa kuboresha Miji na Majiji - TACTIC, ambao Jiji la Arusha ni miongoni mwa majiji yaliyopata neema hiyo, mradi unaotekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
 
Ameitaja miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kiwango cha lami barabara za kuingia na kutoka jijini, ujenzi wa soko la Kisasa stendi ya Kilombero, ujenzi wa stendi ya Daladala, ujenzi wa Standi kubwa ya mabasi yaendayo mikoni, ujenzi na soko la kisasa la Machinga eneo la stendi kubwa, miradi ambayo kimsingi yataathiri baadhi ya maeneo na baadhi ya watu.

Amewataka wafanya biashara hao kukubalina na mabadiliko yanayokuja, mabadiliko ambayo yana lenga kukuza sekta ya uchumi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla wake hivyo ni vema kujiandaa kuyapokea.

"Hapa ilipo stendi ya Daladala linajengwa soko la kisasa la Machinga, ambalo wafanya biasha waliopo sasa ndio watalitumia, stendi itahamia nje ya mji na Daladala zitapita katikati ya Jiji kushusha abaliria tuu, ili kupungumza msongamano wa magari, ambao ni kero kwa wananchi na unachelewesha shughuli nyingi" Ameweka wa Mhe. Mongella.

Aidha ameuagiza uongozi wa Jiji la Arusha kuweka taa kwenye soko la Kilombero ili wafanyabiashara wafanye biashara mpaka usiku na sio kufunga saa 12.













Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link