WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene tarehe 19 Oktoba, 2023 amezindua Mradi wa Kivuko katika Kijiji cha Mkata Mashariki Wilayani Handeni, uliyogharimu jumla ya Tshs. Milioni 11.4.
Mradi huo ni moja kati ya miradi 109 iliyotekelezwa na walengwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF.
Jumla ya wanufaika 56 kati ya 262 wa kijjji hicho wameshiriki katika mradi huu.
Waziri wa Nchi Simbachawene yupo Wilayani Handeni katika ziara yake ya siku moja kutembelea na kukagua wanufaika wa Miradi ya TASAF pamoja na kuzungumza na Watumishi wa Halmashauri hiyo.