Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Tarehe 21/10/2023 ameshiriki matembezi ya hisani kwa ajili ya utambuzi na elimu juu ya Saratani ya Matiti yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar Es Salaam
Waziri Ummy katika matembezi hayo ambapo ameambatana na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Charlotta Azaki pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Afya.
Aidha, Tanzania na Sweden ni nchi ambazo zimekuwa na ushirikiano kwa miaka 60 ya maendeleo ambapo na Sekta ya Afya ni sehemu moja wapo.
Lengo la matembezi hayo ya hisani ni kujenga uelewa kwa wananchi juu ya Saratani ya Matiti ikiwa ni mwezi wa Saratani ya Matiti Tanzania ambapo huadhimishwa kila ifikapo mwezi wa 10.