Hayo yamebainishwa wakati Wataalamu Mbalimbali kutoka Wizara ya Afya wakiwasilisha mada katika Kongamano la 10 la Tanzania Health Summit lililifanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya wa miaka mitano (2021 - 2025) pamoja na Vipaumbele 14 vya Bajeti ya Wizara ya Afya mwaka 2023/2024 ambavyo vimeweka msisitizo katika Ubora wa Huduma za Afya zinazotolewa nchi nzima. Pia, Mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo kuelekea Ubora wa Mifumo ya Huduma za Afya Tanzania pamoja na Wajibu wa rasilimali watu katika kuimarisha huduma za Afya nchini ili kuelekea Bima ya Afya kwa wote.
Washiriki wote walipata fursa ya kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Afya pamoja na mawasilisho ya tafiti za kisayansi.
Kongamano hilo limefungwa leo rasmi ambapo lilifunguliwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiambatana na Waziri wa Afya Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu