Home » » MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AONGOZA MATEMBEZI YA BUNGE BONANZA KWA NIABA YA RAIS WA ZANZIBAR

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AONGOZA MATEMBEZI YA BUNGE BONANZA KWA NIABA YA RAIS WA ZANZIBAR

Written By CCMdijitali on Saturday, June 22, 2024 | June 22, 2024

Published from Blogger Prime Android App

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiongoza matembezi ya Grand Bunge Bonanza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi yaliyoanzia katika viwanja vya Bunge na kumalizia katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussen Ali Mwinyi amesema Serikali zote mbili zitaendelea kuweka mazingira bora ya miundombinu ya michezo nchini itakayowawezesha wanamichezo kufanya michezo yao katika mazingira rafiki ambayo yatapelekea kuibua vipaji vipya vya michezo hasa kwa vijana.

 

Ameyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika Tamasha la Grand Bunge Bonanza lililofanyika katika kiwanja cha Jamhuri Jijini Dodoma.

 

Rais Dk Mwinyi amesema kuwa Serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, Sera na Mikakati mbali mbali zitaendelea kuboresha Sekta ya Michezo ikiwa ni pamoja na kujenga Uwanja wa kisasa wa michezo Dodoma Mjini ambao utajumuisha viwanja vya mpira wa mikono, pete na netiboli ambapo utakapo kamilika utachukua zaidi wa watazamaji elfu thelathini watakao kuwa wamekaa katika viti bila ya usumbufu wa aina yoyote.

 

Amesema kuwa Serikali inaendelea kujenga viwanja vya mazoezi na vya upumzikia katika Jiji la Dodoma utakao jumuisha viwanja vya kisasa vya mpira wa miguu, viwanja vya mpira wa wavu, kikapu, pete, tenis na miundombinu mengine ambapo kwa sasa ujenzi huo umefikia asilimia 41.

 

Aidha amesema kuwa mazoezi yana umuhimu mkubwa katika kuimarisha afya, kujenga umoja na upendo, udugu, nidhamu, ukakamavu na kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kila siku hivyo amewataka Wabunge kuendelea kufanya Tamasha hilo la michozo ambalo linapaswa kuigwa na Taasisi nyengine hapa nchini.

 

Rais Dkt Mwinyi amesema Grand Bunge Bonanza limekuwa likiwahamasisha Wabunge na watumishi wa Ofisi ya Bunge kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya na kuboresha ufanisi wao kiutendaji sambamba na kuendeleza umoja baina ya Muhimili wa Bunge na Baraza la Wawakilishi pamoja na kudumisha na kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao umeshatimia miaka 60 tokea kuasisiswa kwake.

Nae Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa umoja wa Mabunge Duniani Mhe. Dkt Tulia Ackson amesema Tamasha la Grand Bunge Bonanza linatoa fursa ya kufanya mazoezi pamoja na kuifanya miili iwe na Afya na Utayari wa kufanya kazi kwa uweledi na umakini wa hali ya juu.

 

Dkt. Tulia amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga kuboresha na kuimarisha Sekta ya Michezo nchini kwa kutenga bajeti ya zaidi ya shilingi Bilioni mia mbili na themanini (280) ambazo zitatumika katika maboresho hayo.

 
Aidha Mhe. Spika ameipongeza na kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuendelea kushirikiana na Bunge katika kufadhili program mbali mbali za Kimichezo zinazoendeshwa na Bunge jambo ambalo linazidisha umoja, upendo na ushirikiano baina ya Bunge na Taasi mbali mbali nchini.

 
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndugu ABDULMAJID NSEKELA ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha hilo amesema CRDB imekuwa ikifanya kazi kwa karibu sana na Bunge katika shuhuli mbali mbali ikiwemo michezo ambapo wanajivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya Grand Bunge Bonanza ambalo limekuwa likitoa hamasa kubwa kwa wananchi kufanya mazoezi.

 
Nsekela amesema CRDB Benki itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake na kuwa mstari wa mbele katika kutoa ushirikiano na kudhamini program mbali mbali za kimichezo ili kuhakikisha ustawi wa jamii unaimarika na Sekta ya Michezo inaimarika zaidi siku hadi siku.

 
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)


🗓 22.06.2024

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link