Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba kuhakikisha ujenzi wa eneo la Bustani ya Mwanamashungi unakamilika ndani ya wiki mbili zijazo ili kutoa nafasi kwa wananchi kulitumia eneo hilo.
Akikagua maendeleo ya ujenzi wa Bustani hio Makamu wa Pili wa Rais amesema kumekuwa na changamoto ya uhaba wa maeneo ya kupumzukia kwa wakaazi wa maeneo hayo na maeneo jirani ya mji wa chake chake hivyo Baraza la Manispaa wanalazimika kuchukua jitihada za ziada kuhakikisha mkandarasi anamaliza ujenzi huo kwa wakati na viwango vinavyotakiwa ili wananchi waweze kunufaika na bustani hio.
Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar amesema kukamili kwa bustani hio itawanufaisha wananchi hasa wajasiriamali wadogo wadogo kwa kuweza kufanya biashara zao maeneo hayo kwa lengo la kujipatia kipato kwa mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa Taifa.
Aaidha makamu wa Pili wa Rais ameagiza kuzungushiwa uzio eneo lote linalozunguka bustani hio kwa ajili ya usalama wa wananchi watakaofika katika bustani hio wao na mali zao.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais amekagua ujenzi wa maegesho ya magari pamoja na ujenzi wa nyumba za makaazi na maduka zinazojengwa na Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC)katika eneo la Mabatini chake chake ambapo amesema miradi yote inayojengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina maslahi makubwa kwa wananchi kwani kukamilika kwa ujenzi wa nyumba hizo kutapunguza changamoto ya makazi kwa wananchi na wafanyabiasha watafanya biashara zao katika maeneo rasmi.
Pia ameawataka wafanya biashara kuacha tabia ya kufanya biashara pembezoni mwa barabara jambo linaloleta usumbufu kwa watumiaji wa barabara hizo na kuisababishiaa hasara kubwa serikali .
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar amesema kituo cha maegesho ya magari kinachojengwa Tibirinzi kitakapokamilika kitatatua kero ya msongamano wa magari ndani ya mji wa chake-chake na kutoa fursa kwa wafanyakazi kuegesha magari yao katika maeneo salama.
Nae Naibu waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Salha Mohd Mwinjuma amesema Wizara itasimamia na kuhakikisha ujenzi wa nyumba hizo uliojumiisha na Nyumba za Makaazi na Milango ya maduka unakamilika kwa wakati uliopangwa na kwa kiwango kilicho kusudiwa ili kuwawezesha wananchi kuishi sehemu salama sambamba na wafanya biashara kuweza kuendelea na biashara zao ndani ya jengo hilo.
Aidha Mhe. Salha ameiomba Serikali kuwapatia eneo lililopo pembezoni mwa nyumba hizo ili waweze kuendelea na ujenzi mwengine wa nyumba ili kuhakisha wanaunga mkono jitihada za Mhe.Rais za kuwaletea wananchi maendeleo ikiwemo kuwajengea nyumba za kisasa za bei nafuu.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chake - Chake Mhe. Ramadhan Suleima Ramadhan amesema kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Bustani ya Mwanamashungi na miradi mengine inayojengwa na serikali kutaubadilisha muonekano wa mji wa chake na kuwa wa kisasa zaidi na wananchi watapata fursa ya kufanya biashara zao katika eneo hilo.
Amesema wananchi wa Jimbo la Chake - Chake wataendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dkt Mwinyi ambe amedhamiria kuifungua Pemba kiuchumi na kimaendeleo na kuahidi mwaka 2025 kumpigia kura nyingi ili aendeleo kuiongoza Zanzibar kwa mafanikio zaidi.
Miradi iliyokaguliwa na Mhe. Makamu wa Pili wa Rais ni pamoja na UJENZI WA MAEGESHO YA MAGARI TIBIRINZI, UJENZI WA BUSTANI YA MWANAMASHUNGI, UJENZI WA MRADI WA NYUMBA ZA MAKAAZI NA MADUKA MABATINI, UJENZI WA OFISI ZA WIZARA YA ELIMU PEMBA NA UJENZI WA SKULI YA MSINGI YA MICHAKAINI "B" YA GOROFA (G+2).
Imetolewa na kitengo cha habari (OMPR)
Leo tarehe 01.08.2024.