Home » » WANAODAIWA KODI YA PANGO LA ARDHI WATAKIWA KULIPA IFIKAPO DESEMBA 31, 2024

WANAODAIWA KODI YA PANGO LA ARDHI WATAKIWA KULIPA IFIKAPO DESEMBA 31, 2024

Written By CCMdijitali on Thursday, December 19, 2024 | December 19, 2024

 NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geophrey Pinda amewaelekeza watendaji wote wa sekta ya ardhi nchini, kuratibu na kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa mkakati wa ulipaji wa kodi ya pango la ardhi kwa kila mwaka.


Mhe Pinda ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mkutano wake na wandishi wa habari Desemba 19, 2024 jijini Dodoma.

“Katika kipindi hiki kilichobaki, vituo vya makusanyo ambavyo ni Ofisi za Ardhi za Mikoa na Ofisi za Ardhi za Halmashauri zote nchini, zitakuwa wazi hadi muda wa saa kumi na mbili (12:00) jioni” amesema Pinda.


Mhe Pinda ametoa rai kwa wamiliki wote wa ardhi wanaodaiwa Kodi ya Pango la Ardhi kuhakikisha wanalipa hadi kufikia Desemba 31, 2024 ambapo kila mmiliki wa ardhi amepewa sharti la kulipa kodi ya pango la ardhi kwa kila mwaka kwa mujibu wa sheria kila kwa mujibu wa Kifungu cha Kifungu cha 24A cha Sheria ya Ardhi (Sura ya 113).

“Kila mmiliki wa ardhi ambaye ardhi yake imepimwa anapaswa kuwasilisha maombi ya kumilikishwa ardhi husika ndani ya muda wa siku 90 kuanzia tarehe ya kuidhinishwa kwa ramani ya upimaji wa ardhi yake. Baada ya muda huo kupita mmiliki anawajibika kuanza kulipa kodi ya pango la ardhi kwa kuzingatia sheria za ardhi.

Hivyo, nawakumbusha wamiliki wote wa ardhi nchini ambao ardhi wanazomiliki zimepangwa na kupimwa, kutekeleza takwa hilo la sheria kwa kuwasilisha maombi ya kumilikishwa ardhi na kuanza kulipa kodi ya pango la ardhi,” amesema Mhe Naibu Waziri Pinda.







Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link