Mafunzo hayo yameanza kutolewa rasmi leo 19.12.2024 katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Herring Christian, yametolewa na Wakufunzi ambao ni wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Yaliyohusisha kata ya Chimala,Itamboleo na Ihahi.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe,Col Maulid H.Surumbu amesema kuwa niwajibu wakila kiongozi kuwajibika katika sehemu yake kwa kusikiliza kero za Wananchi na kutambua mipaka yake kwenye Uongozi.
Vile vile ametaja vipaumbele vinavyopaswa kuzingatiwa na viongozi wa awamu hii ambavyo ni:-
"Posi zifanye kazi zilizokusudiwa katika ukusanyaji wa Maputo, kutatua kero za Wananchi kwa wakati,Usalama kati ya Mkulima na Mfugaji,usimamizi wa Miradi ya maendeleo usafi na utunzaji wa mazingira".Amesema Col Surumbu.
Naye Modesta Ngoroma ambaye ni Afisa Sheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali amewaelezea utaratibu wa kutunga Sheria ndogo na utatuzi wa migogoro vijijini.
"Halmashauri ya kijiji itapendekeza Aina ya sheria inayotakiwa kutungwa na itawasilishwa na kwenye mkutano mkuu wa kijiji ili kupata maoni ya wanakijiji wote pia Halmashauri ya Wilaya ikiridhia mapendekezo hayo itadhinisha sheria hiyo ndogo na baada ya hapo itakuwa tayari kutumika". Amesema Modesta
Vumilia Rajabu Mwahibewile mbaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Isitu, amesema kuwa" Asanteni kwa mafunzo haya mimi kama kiongozi nimeelewa kanuni,Sheria na taratibu zote za uongozi hakika nitawaongoza vizuri Wananchi wangu kwa kusikiliza kero na kuzitatua.