Home » » RAIS MWINYI AISHUKURU WB KWA MSAADA WA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR

RAIS MWINYI AISHUKURU WB KWA MSAADA WA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR

Written By CCMdijitali on Tuesday, February 18, 2025 | February 18, 2025

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Benki ya Dunia kwa Msaada wa kiasi cha Dola Milioni 100 kwa ajili kuimarisha Miundombinu ya Sekta ya Afya  hapa nchini.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Mwa Afrika  Milena Stefanova na ujumbe wake, Ikulu Zanzibar tarehe 18 Februari 2025.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameuelezea Ujumbe huo kuwa Serikali ina Malengo Mahsusi ya kuifanya Zanzibar kuwa kituo Bora cha Matibabu kwa Nchi za Afrika Mashariki na Afrika  kwa  Ujumla na kuipongeza Benki ya Dunia kwa kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.

Naye Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini Mwa Afrika Milena Stefanova ameeleza kuwa Benki hiyo inaridhika na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya  Zanzibar za kuimarisha huduma za Afya na kuahidi kuendelea na misaada kwa ustawi wa watu wake.

Kwa upande mwingine Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazroui ameeleza kuwa Wizara hiyo inajipanga  vema  kuhakikisha fedha hizo zinaenda kutumika kufanikisha  lengo la kuifanya Zanzibar kuwa kituo cha pekee cha Utalii waTiba na  Matibabu na Mafunzo ya Afya ( HEALING ISLAND)kama zilivyo nchi za India na THailand









 

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link