Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Elias Magosi pembezoni mwa Kikao cha 46 cha Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika kilichofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 13 na 14 Februari, 2025.
Mazungumzo ya viongozi hao yaliangazia juu ya umuhimu wa kuimarisha ushirikiano ili kujenga mtangamano imara wenye amani na usalama ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kukuza uchumi katika kanda ya SADC na Afrika kwa ujumla.
Aidha, Waziri Kombo amempongeza Mhe. Magosi kwa ushindi uliopatana kwa kanda ya kusini kufuatia uchaguzi uliofanyika katika kikao hicho cha Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika ambapo ukanda huo umefanikiwa kuibuka na ushindi wa nafasi tano (5) katika taasisi za Umoja huo.
Pamoja na masuala mengine viongozi hao pia wamejadili juu ya mandalizi ya mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika pembezoni mwa Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika Addis Ababa, Ethiopia.