Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amesema maendeleo yanayoonekana Nchini yanatokana na umoja na Mshikamano wa Wananchi bila ya kujali tofauti zao.
Alhajj Hemed ameyasema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka Mikoa miwili ya Pemba katika Iftar aliyoiandaa kwa Wananchi hao iliyofanyika katika viwanja vya kufurahishia watoto Tibirinzi Wilaya ya chake-chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Amesema Serikali inayoongozaa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi inaendelea kusisistiza umoja na Mshikamano ambavyo ndio Nguzo pekee ya kufikia azma yake ya kuwaletea maendeleo Wananchi wake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Miradi inayojengwa na Serikali inaelekezwa Unguja na Pemba kama vile Skuli, Hospital, Miundombinu ya Maji, Barabara, Miradi ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi ili kuweka usawa kwa Wananchi wa pande zote mbili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewashukuru Wananchi kwa kuitikia mualiko huo na kuungana nae ambapo amesema Kitendo hicho ni cha kiungwana na kinaonesha mapenzi na umoja uliopo Baina ya Wananchi na Viongozi.
Akitoa Shukurani kwa Niaba ya Wananchi hao Bwana Muhammad Nassor Salim amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kuendeleza utamaduni wa kufutari pamoja na Wananchi na kueleza kuwa suala hilo ni la kuigwa na ni Ibada yenye Fadhila kubwa mbele ya Allah (S.W)
Amesema Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba wameridhika na maendeleo yanayoonekana Nchini yanayotokana na unawajibikaji katika Kila Idara katika kuwatumikia Wananchi wa Zanzibar.
Imetolewa na Kitengo cha Habari(OMPR)
Tarehe 12.03.2025